Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka
Kampuni ya kikandarasi ya Sumitomo Mitsui inayojenga mradi wa ujenzi wa
barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na
Mandela eneo la Tazara kumaliza ujenzi huo kwa wakati mradi huo ili
kusaidia kupunguza tatizo la msongamano.
Akizungumza
mara baada kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo jijini Dar es
salaam, Profesa Mbarawa amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutajenga
historia nchini kutokana na kuwa ni wa mwanzo kujengwa.
“Nimefurahi
kuona mradi huu upo katika hatua nzuri, naomba mkamilishe mradi huu
unakamilika kwa ubora na kwa wakati ili tatizo la msongamano lililopo
katika maeneo haya kupungua au kuisha kabisa,” amesema Waziri Mbarawa.
Profesa
Mbarawa amemtaka Mkandarasi kuhakikisha kuwa anafanya kazi kwa umakini
na kwa uangalifu wakati wa kipindi chote cha ujenzi ili kuitokuweza
kusababisha foleni katika eneo hilo.
Aidha,
Waziri Mbarawa amewataka wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa
Mkandarasi huyo ili kurahisisha kazi za ujenzi huo kukamilika kwa wakati
na kupata matokeo chanya.
“Nawaomba
watanzania wenzangu kuwa wavumilivu na usumbufu wowote utakaojitokeza
katika kipindi hiki chote, kwani ukamilifu wa mradi huu utasaidia
kupunguza tatizo la msongamano katika barabara hizi,” amefafanua Waziri
Mbarawa.
Katika
hatua nyingine, Profesa Mbarawa amekagua daraja la watembea kwa miguu
eneo la Buguruni Sheli na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kulitunza
daraja hilo ambalo uwepo wake umesaidia kupunguza ajali katika maeneo
hayo.
“Ni
matumaini yangu sasa wakazi wa maeneo haya mtavuka kwa amani kupitia
daraja hili, na ajali zilizokuwa zikitokea maramara hazitakuwepo tena”,
amesema Profesa Mbarawa.
Kwa
upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng.
Patrick Mfugale amemuahidi Waziri huyo kumaliza kwa wakati ujenzi huo
na kumhaakikishia Waziri kuwa ujenzi wa barabara hiyo utakuwa na viwango
vilivyo bora.
Mradi
wa Tazara Flyover ni msaada kutoka Serikali ya Japan ambao umegharimu
shilingi bilioni 93.4 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka 2018.
|
September 30, 2016
WAZIRI MBARAWA AMTAKA MKANDARASI ANAYEJENGA FLYOVER YA TAZARA KUMALIZA KWA WAKATI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment