WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajia kuhamia rasmi Dodoma leo.
Majaliwa
anahamia mjini hapa ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ahadi ya Serikali ya
awamu ya tano ya kuhamia Dodoma ambako ndiko yaliko makao makuu ya nchi.
Julai
25 mwaka huu, katika kilele cha siku ya mashujaa kilichofanyika mkoani
hapa, Waziri Mkuu Majaliwa alisema ifikapo Septemba mwaka huu, Serikali
itakuwa imehamia mjini hapa.
Hatua hiyo ya waziri mkuu ilitangazwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alipozungumza na waandishi wa habari.
Alisema Waziri Mkuu anatarajiwa kuwasili leo mchana akitokea Dar es Salaam alikokuwa akiishi.
“Baada
ya kuwasili hapa atafanya ziara ya siku mbili katika Manispaa ya
Dodoma Oktoba mosi na Oktoba 2 mwaka huu kukagua hatua mbalimbali za
maandalizi ya kupokea Serikali mkoani hapa.
“Wakati
wa ziara hiyo, atakagua majengo ya Serikali, maeneo ya kutolea huduma
za afya, kituo cha umeme cha Zuzu, masoko, chanzo cha maji Mzakwe na
maeneo ya viwanda.
“Kwa
hiyo maandalizi yote muhimu kwa ajili ya mapokezi ya waziri mkuu
yamekamilika na uongozi wa mkoa unaendelea kuwajulisha wananchi na wadau
wote katika maeneo yatakayohusika na ziara hiyo, washiriki kwa
ukamilifu.
No comments:
Post a Comment