RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo , Joseph Kabila akiungumza Ikulu leo.
…………………………………………………………………..
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo , Joseph Kabila amesema Serikali yake itaendelea kutumia
bandari ya Dar es Salaam kupitishia mizigo yake ili kuendeleza
ushirikiano na manufaa ya kiuchumi baina ya wananchi wa nchi hizo.
Akizungumza na waandsihi wa
habari leo Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya mazungumzo
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli, alisema
kuwa nchi ya Kongo imekua ikitumia Bandari ya Dar es Salaam tangu
hapo awali, na sasa wanatarajia kutumia bandari hiyo kwa kupitisha
mizigo zaidi.
“Tunatarajia kufanya biashara
zaidi na Bandari ya Dar er salaam kwa kupitisha mizigo kwa wingi, miaka
ya nyuma tulikua na matataizo kidogo ila kwa sasa kuna kazi kubwa
inafanyika ya kuboresha Bandari ya Dar es salaam na sisi tutaweza
kupitisha mizigo yetu kwa wingi” alisema Rais Kabila.
Aidha Rais Kabila alisema kuwa
katika mazungumzo yake na Rais Magufuli walijadili masuala mbalimbali
ikiwemo hali ya usalama katika mipaka ya Kongo na uwekezaji.
Kwa upande wake Rais Magufuli,
alisema kuwa katika kuboresha usafirishaji mizigo kwenda nchini Kongo,
Bandari ya Dar es salaam imepunguza maeneo ya vituo vya kupima mizigo
ambapo kwa sasa kuna maeneo matatu yenye vituo vya kupimia mizigo
ambavyo ni Vigawanza, Manyoni na Nyakaliwa.
Ambapo pia Bandari hiyo imeongeza
kipindi cha msamaha wa kuhifadhi mizigo bandarini kutoka nchini Kongo
kutoka siku 14 hadi siku 30.
Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa
biashara kati ya Tanzania na Kongo imendelea kuimarika hadi kufikia
shilingi bilioni Tsh. 393.6 kutoka Tsh. Bilioni 23.1 kwa mwaka 2009.
Katika hatua nyingine, Waziri wa
Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo na Waziri wa Mafuta wa Kongo
Mhe. Ngoyi Makena wametia saini mkataba wa makubaliano wa kutafuta
mafuta katika ziwa Tanganyika.
Ziara ya Rais wa Kongo nchini
inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia pamoja na kukuza maendeleo
ya uchumi baina ya nchi hizo mbili.
No comments:
Post a Comment