Vigogo ambao pia ni mahasimu wa soka Tanzania bara kutoka mtaa wa
kariakoo jijini Dar es salaam, Yanga na Simba,leo watapambana katika mechi ya kwanza ya
ligi kuu ya soka ya Tanzania bara a.k.a Ligi ya Vodacom itakayopigwa katika uwanja mkuu wa
taifa jijini Dar es salaam. Timu hizo zilikuwa kambini kujiandaa kwa mechi hiyo ,Simba mpaka sasa ndio wanaongoza ligi
baada ya kucheza Mechi 6 na wana pointi 16 wakifuatiwa na Stand United
wenye Pointi 12 kwa Mechi 6. Nafasi ya tatu ni Yanga huku nafasi za nne
na tano zipo Azam FC na Mtibwa Sugar zote zikiwa na pointi 10 kila
mmoja. Katika kuelekea mechi hiyo makocha wa timu hizo Joseph Omong wa simba na Hans van Pluijim, kila mmoja amesema kuwa timu itaibuka na ushindi. Msimu uliopita, Yanga iliikung'uta Simba mabao 2-0 katika mechi zote mbili. |
October 1, 2016
HATAREEE! LEO NI LEO UWANJA WA TAIFA SIMBA VS YANGA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment