Multichoice
yakabidhi vifaa maalum vya michezo kwa watu wasioona ambavyo
vitawawezesha kuhudhuria maadhimisho ya siku ya kimataifa ya fimbo
nyeupe tarehe 06/10/2016 itakayofanyika mkoani Mbeya. Lengo kuu la
maadhimisho hayo ni kuhamasisha jamii na watumiaji wa barabara,
kuiheshimu fimbo nyeupe, na kumsaidia asiyeona anapotembea na
anapohotaka kuvuka barabara.
Vifaa
vilivyotolewa ni: Mipira (4) ya goalball, Domino set nne, Karata nne,
fedha za nauli na kujikimu kwa timu hiyo ya wasioona. Mchango huo wa
Multichoice unathamani ya jumla ya shilingi 3,120,000/=. Akitoa msaada
huo mkurugenzi mkuu wa Multichoice Tanzania Maharage Chande alisema
“Multichoice inafuraha kubwa kushirikiana na nduguzetu wasioona wa Dar
es salaam katika kuwaandaa kushiriki maadhimisho yatakayofanyika Mbeya,
kama kampuni ya kitanzania tutaendelea kuwa mstari wa mbele kushirikiana
na jamii yetu kila fursa inapojitokeza”.
Kampuni
ya MultiChoice Tanzania inaomgoza kwa kutoa burudani za michezo na
filamu kwa kupitia DSTV. Makao makuu yake ni Dar es salaam na Inamatawi
Mwanza, Arusha, na Mbeya.
|
October 1, 2016
MULTCHOICE YAWAKUMBUKA WASIOONA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment