- Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba (kushoto) akikata
keki maalum kuashiria uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja Ubungo
jijini Dar es Salaam leo. Kituo hicho kipya pamoja na duka la bidhaa za
kampuni ya TTCL kipo katika Jengo la Ubungo Plaza la jijini Dar es
Salaam.
- Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja cha
Kampuni
ya Simu Tanzania (TTCL), Ubungo leo jijini Dar es Salaam. Kituo hicho
kipya pamoja na duka la bidhaa za kampuni ya TTCL kipo katika Jengo la
Ubungo Plaza la jijini Dar es Salaam.
- Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja TTCL, Leonard Lubu akizungumza na wanahabari mara baada ya uzinduzi.
- Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba (kushoto) akikata
keki maalum kuashiria uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja Ubungo
jijini Dar es Salaam leo. Kituo hicho kipya pamoja na duka la bidhaa za
kampuni ya TTCL kipo katika Jengo la Ubungo Plaza la jijini Dar es
Salaam.
- Mkuu
wa Biashara wa Kampuni ya TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bi. Jane
Mwakalebela (kushoto) akimlisha kipande cha keki Kaimu Afisa Mtendaji
Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba kwenye hafla hiyo.
KAMPUNI ya
Simu Tanzania (TTCL) leo imezinduwa kituo kipya cha huduma kwa wateja
kilichopo katika Jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, kituo
kitakacho toa huduma kwa wateja mbalimbali wa kampuni hiyo pamoja na
wananchi wengine wanaoitaji huduma za TTCL.
Akizinduwa
kituo hicho, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba
alisema uzinduzi huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa shughuli mbalimbali
katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka 2016, ikiwa na
lengo la kutambua mchango wa wateja kutumia huduma za kampuni hiyo na
kuchangia maendeleo ya kampuni hiyo na taifa kwa ujumla.
Kindamba
alisema uzinduzi wa kicho hicho cha huduma kwa wateja hasa wa eneo la
Ubungo ni sehemu ya mpango wa TTCL katika kuboresha vituo na maduka yake
nchi nzima ili yaweze kutoa huduma bora na kwa ufanisi zaidi. Alisema
kutokana na mahitaji ya wateja, TTCL imedhamiria kuongeza idadi ya vituo
hivyo pamoja na maduka yake ikiwa ni mpango wa kusogeza zaidi huduma
kwa wateja maeneo anuai.
"Kituo
hiki cha huduma kwa wateja cha Ubungo ambacho kinazinduliwa leo,
kitahudumia wateja kutoka katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es
Salaam. Eneo hili la Ubungo ni lango la kuingia katikati ya jiji huku
maeneo yanayozunguka yakiwa na idadi kubwa ya watu, hivyo tunategemea
kupata wateja wengi wanaoingia jijini Dar es Salaam pamoja na wanaoishi
maeneo ya jirani ikiwemo Sinza na Mabibo..," alisema.
- Meneja
wa TTCL Mkoa wa Dar es Salaam-Kaskazini, David Dirisha (kulia)
akimuongoza Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba
(katikati) kutembelea kituo hicho. Kushoto ni Bi. Jane Mwakalebela.
- Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba (kulia) akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kuzinduwa kituo hicho cha huduma.
Kushoto ni Mkuu wa Biashara wa kampuni hiyo kanda ya Dar es Salaam, Bi.
Jane Mwakalebela.
Aidha
aliongeza kuwa kutokana na maboresho makubwa ambayo kampuni hiyo ya
kizalendo imeyafanya imejipanga kufanya kazi kwa ufanisi na kutekeleza
falsafa ya Serikali ya Awamu ya Tano ya 'Hapa Kazi Tu, huku ikitumia
rasilimali za nchi vizuri na kuchangia mageuzi yanayoendelea nchini ya
kuifanya Tanzania kupiga hatua kuelekea nchi ya uchumi wa kati na nchi
ya viwanda.
Kituo
hicho kipya kitatoa huduma mbalimbali zikiwemo kuunganisha wateja wa
huduma za intaneti, kurejesha namba iliyopotea, kufanya malipo ya ankara
za huduma za TTCL, kusajili namba za simu za 4G, kuuza muda wa
maongezi, kuuza modemu zenye ofa kabambe, kupata Routers na kuunganishwa
na huduma za T-TV inayowezesha wateja kutazama matangazo ya vituo vya
luninga moja kwa moja kupitia simu zao za mkononi na vifaa vingine vya
kisasa vya mawasiliano
No comments:
Post a Comment