Kaimu Kamishna Mkuu TRA, Mary Maganga.
Katika
kuhakikisha inaboresha huduma kwa wafanyabiashara ambao wanaingiza
mizigo nchini kwa njia ya bandari, mipaka na viwanja vya ndege, Serikali
kupitia Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imeeleza mpango wa Serikali wa
kuanza kutumia mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window
System) ambao kwa hakika utamaliza tatizo la mizigo kukaa muda mrefu
kwa sababu ya kukosekana vibali.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kumalizika mafunzo ya siku moja kuhusu
mfumo wa Dirisha Moja la Huduma kwa taasisi zinazotoa vibali na
wafanyabiashara, Meneja Mfumo wa Kieletroniki wa Dirisha Moja la Huduma,
Tinka Felix alisema lengo la kuanza kutumia mfumo huo ni kuboresha
huduma ambazo wanazitumia sasa ili wafanyabiashara wanaoingiza mizigo
nchini waweze kuipata kwa haraka kuliko ilivyo sasa.
|
Meneja
Mfumo wa Kieletroniki wa Dirisha Moja la Huduma, Tinka Felix
akizungumza kuhusu mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single
Window System). (Picha zote na Rabi Hume – MO DEWJI BLOG)
“Ni
mpango wa Serikali kuboresha huduma kwa wateja kwa kupunguza muda wa
kutoa mizigo bandarini au mipakani au kwenye viwanja vya ndege, kupitia
mfumo huu wateja hawatakuwa wakienda kwenye idara na taasisi za Serikali
na badala yake wakiwa hukohuko kwenye ofisi zao wataweza kuomba na
kupata vibali na kupata bili za malizo kwenda kulipa benki, mfumo pia
utafanya kazi na benki,” alisema Felix.
Alisema
Tanzania haitakuwa nchi ya kwanza kutumia mfumo huo na mataifa mengi
yanautumia ili kurahisisha huduma kutolewa kwa haraka kwani mfumo wa
sasa wa forodha (tancis system) unashindwa kufanya kazi kwa haraka jambo
ambalo linasababisha mizigo kuchelewa kutolewa kutokana na muda mrefu
mmiliki kutumia kutafuta vibali.
|
Mkurugenzi
wa Sera Utafiti Na Ushauri wa TPSF, Gili Teri akizungumza faida za
kutumia mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window
System).
“Mfumo
wa sasa ili mtu apate kibali anatakiwa atembelee hizo ofisi hata mara
10 na baadhi ya ofisi wanataka vibali zaidi ya kimoja lakini mfumo huu
wa sasa muda ambao unatumika kuomba vibali utapungua na tunategemea
kuokoa Dola milioni 65 kwa kutumia tu mfumo wa electronic single window
system,” alisema Felix.
Alisema
kwa sasa kuna taasisi za Serikali 47 ambazo zinatoa vibali lakini mfumo
wa Dirisha Moja la Huduma utatumiwa na taasisi 32 ambazo kwa pamoja
zitakuwa zikitoa vibali 106.
Aidha
alisema Serikali imeagiza kuwa mfumo huo uanze kutumika baada ya mwaka
mmoja hivyo wanategemea kuanzia mwakani mfumo ambao watakuwa wakitumia
utakuwa ni wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System)
ambao utawezesha wafanyabiashara ambao wanatoa mizigo kupitia bandari,
mipaka au viwanja vya ndege kupata vibali kwa haraka.
|
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo ya siku moja wakiuliza maswali na kutoa maoni kuhusu mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System). |
No comments:
Post a Comment