WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amefungua duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD)
katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda lililogharimu sh. milioni 55
litakalohudumia mikoa mitatu ya Kigoma, Katavi na Tabora.
Pia
duka hilo itatoa huduma kwa vituo vya kutolea huduma za afya 580 ikiwa
ni pamoja na hospitali za rufaa za mikoa miwili ya Kigoma na Tabora,
Hospitali za wilaya sita za Nzega, Igunga, Urambo, Kobondo, Kasulu na
Mpanda Mji.
Waziri Mkuu amefungua duka hilo la dawa la MSD, lililoko katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi jana (Jumanne,
Januari 17, 2017) ikiwa ni utekelezaji wa agizo alilolitoa kwa MSD
Agosti 20, 2016 alipokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Katavi.
Aliuagiuza uongozi MSD kujenga duka hilo ili kurahisisha upatikanaji wa
dawa katika mkoa huo pamoja na mikoa jirani.
Aidha,
Waziri Mkuu amesema baada ya kufunguliwa kwa duka hilo Serikali
haitarajii kusikia tena katika vituo vya afya na Zahanati zilizoko
mkoani Katavi na mikoa jirani zinakosa dawa. Amewaagiza Wakurugenzi
kusimamia suala hilo na kuhakikisha vituo vyote vya afya vinakuwa na
dawa za kutosha.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Afya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kukutana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kutafuta namna bora ya kutumia fedha
za huduma za afya zinazipatikana katika halmashauri nchini.
Aidha,
Waziri Mkuu amesema Serikali imetoa sh. bilioni 1.5 kwa ajili ya kuanza
ujenzi wa hospitali ya mkoa wa Katavi ili kupunguza msongamano wa
wagonjwa katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda.
Amesema
lengo la Serikali ni kuwa na Hospitali ya Rufaa kwa kila mkoa, hivyo,
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa mipya itakayojengwa Hospitali ya
Mkoa ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Laurean Bwanakunu alisema
ujenzi waduka hilo la Mpanda hadi kukamilika umegharimu sh. milioni 55,
huku benki ya CRDB ikitoa sh. milioni 50 na MSD imeweka dawa na vifaa
tiba vya sh. milioni 104.45 na vifaa vya TEHAMA vya sh. milioni tano.
Alisema
kuanzishwa kwa duka hilo kutaongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba
kwa wagonjwa hasa dawa ambazo hazimo katika orodha zilizoidhinishwa na
Serikali kutumika katika vituo vyake vya kutolea huduma za afya ila
zimeidhinishwa kutumika nchini na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Alisema
dawa na vifaa tiba vilivyomo katika orodha ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) zinapatikana katika duka hilo kwa bei nafuu, hivyo kuondoa
usumbufu kwa wagonjwa kwenda kuzitafuta katika maduka ya mbali na kwa
bei ghali.
“Nitoe
mfano mdogo wa tofauti ya dawa katika ya maduka ya MSD na maduka ya
mitaani, hapa dawa ya sindano ya kutibu fungus aina ya Fluconazole
inauzwa sh. 2,300 na mitaani sh. 4,500 na dawa ya sindano kwa ajili ya
kushusha kisukari (Insulin) chupa moja MSD ni sh. 8,500 na mitaani sh.
20,000,” alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
|
No comments:
Post a Comment