Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Korogwe Vijijini,Martha Kusare kulia akipokea msaada wa sola ya mobisol kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya
Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka ikishirikiana na A Better World kutoka Canada kwa shule ya sekondari ya Patema ili kuweza kutumia nishati ya umeme kwa ajili ya matumizi yao ambapo sola hiyo na ujenzi wa maabara tatu zilizojengwa na taasisi hiyo iligharimu kiasi cha sh.milioni 75 |
Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka wa pili kulia akiangalia namna wanafunzi wa shule ya sekondari Patema wanayofundishwa masomo ya sayansi mara baada ya kukamilika maabara hiyo |
Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka kulia akiteta jambo na mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Patema,Jerome Massawe |
Muonekano wa Majengo ya maabara hizo |
WATUMISHI katika Halmashauri ya
wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wameonywa kuacha kutumia vibaya fedha za miradi zinazotokana na wafadhili kwenye maeneo yao kwani watakaobainika kufanya hivyo watashughulikiwa ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert
Gabriel wakati akipokea taarifa ya
umalizaji wa majengo ya matatu ya maabara yalijengwa na taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha ikishirikiana na A Better World kutoka Canada kwa shule ya sekondari ya Patema iliyopo kata ya Mpale Wilayani humo.
Aidha wao kama viongozi wa serikali wilayani humo hawatakuwa na
mdhara
na watumishi ambao watabainika kuihujumu
miradi ya maendeleo inayopelekwa kwenye maeneo yao na wafadhili mbalimbali kwani kufanya hivyo kunachangia kurudisha nyuma kasi ya ukuaji wa maendeleo.
“Nisema wazi kuwa watumishi badilikeni kwani mimi kama kiongozi wa
wilaya hii sitamfumbia macho mtu yeyote
ambaye atakuwa kikwazo cha maendeleo kwenye wilaya hii na niwaonye wenye tabia kama hiyo waiache mara moja.
Aidha alisema lazima watu wabadilike hasa wale wanaopewa majukumu
ya
kusimamia miradi hiyo kutoka kwa
wafadhili na wawe wawazi wakati wa utekelezaji wake ili kujenga heshima kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
“Baadhi yetu tunatumia fursa hizo vibaya na kujinufaisha kupitia
fedha
za wafadhili kinyume na hitaji
husika,kufanya hivyo kunaweza kuwakimbiza wadau hao wa maendeleo na kutia doa kwa Taifa”Alisema Gabriel.
Awali akizungumza katika kikao hicho Afisa Elimu sekondari
Halmashauri
ya Korogwe Vijijini Patricia Mbigili
alisema pamoja na jitihada kubwa ambazo wanazifanya kuhakikisha wanakamilisha suala la maabara lakini mpaka sasa zilizokamilika ni 5 kati ya 78 katika shule 26,ambapo kunahitajika maabara 3 kwa kila shule ikiwa ni za chemia,physician na bioligia.
Alisema ili kukabiliana na tatizo la ufaulu wa masomo ya sayansi
katika shule za sekondari maabara na uwepo wa walimu wa masomo hayo unahitajika kwa kiasi kikubwa ili kuweza kuwajengea uwezo wanafunzi kujifunza kwa vitendo.
Mbigili alisema jukumu la kuboresha miundombinu ya shule na makazi
ya
walimu ni la wananchi wote,serkali na
taasisi zinazojitolea ili kutimiza azma ya serikali ya kuboresha sekta ya elimu kama ilivyoanza kwa madawati na elimu bure.
Naye kwa upende wake, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Azidu Kaoneka
alisema umaliziaji wa maabara 3,nyumba 1
ya walimu na kuwawekea kifaa cha kuzalisha umemekupitia jua (mobisol) ambapo kiasi cha shilingi milioni 75 zimetumika.
Azidu alisema taasisi hiyo inaimani kubwa kwa kushirikiana na wananchi
pamoja na serikali wanaweza kujenga
mazingira rafiki ya walimu na wanafunzi kwa kuboresha miundombinu ya mashule pamoja na nyumba za walimu kama ilivyofanyika shuleni hapo. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha. |
No comments:
Post a Comment