Naibu
Waziri wa Afya, Ustawi wa jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis
Kigwangala, ametoa maagizo mazito kwa Vyombo vya Usalama nchini
kuhakikisha vinamkamata mtu anayejulikana kwenye mitandao ya kijamii
kama James Delicious kufuatia kujitangaza kwake kama shoga kinyume cha
sheria ya Tanzania.
Dk.
Kigwangalla ametoa kauli hiyo jana jioni mjini Dodoma Bungeni wakati
akijibu hoja za wabunge juu ya hatua kwa mtu anayefanya vitendo hivyo
ambapo ameviagiza vyombo vya usalama kumtafuta mtu huyo na iwe fundisho
kwani ni kinyume na sheria za nchi kwa kuendesha biashara ya kuuza
ngono ya kinyume cha maumbile.
Mbali
na James Delicious, wengine ambao ameagiza wajisalimishe wenyewe kituo
cha Polisi Central Dar es Salaam ni pamoja na Kaoge Mvuto na Dani Mtoto
wa Mama ambao wamekuwa wakijinadai kufanya vitendo hivyo hapa nchini
ambavyo ni kinyume na sheria.
KIGWANGALLA: Serikali kupiga Marufuku Matumizi ya Pombe za VIROBA Kufikia Mwezi wa Sita mwaka 2017.
Wakati
huo huo, akiendelea kujibu maswali amebainisha kuwa Serikali itazuia
viroba kutengenezwa nchini na kufuta kabisa matumizi ya pombe za aina ya
viroba hapa nchini wakati akijibu hoja za wabunge kufuatia michango
mbalimbali ya wabunge juu ya hoja za Kamati za UKIMWI na Madawa ya
Kulevya na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya jamii.
Dk.
Kigwangalla alisema, ‘haitopita mwezi wa sita Serikali itakuwa imepiga
total ban (marufuku) matumizi ya madawa ya kulevya nchini….’
Miezi
kadhaa iliyopita Dk. Kigwangalla aliongoza kikosi kazi cha Serikali
kilichokuwa kinashughulikia suala la viroba ili kutathmini ukubwa wa
tatizo na kupendekeza hatua za kuchukua.
Kikosi kazi kilibaini changamoto nyingi ikiwemo ya uwepo wa viwanda bubu na pombe zinazochanganywa na spirit ya viwandani.
|
February 7, 2017
DK.KIGWANGALLA AAGIZA KUKAMATWA KWA MTU ANAYEJIITA JAMES DELICIOUS KWA KUJITANGAZA SHOGA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment