Vita
ya kupambana na dawa za kulevya nchini iliyopamba moto zaidi na kuzua
mijadala tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipoanza
kutaja majina ya watuhumiwa imemuibua Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema,
Dkt. Wilbroad Slaa.
Dkt.
Slaa ameibuka baada ya kutajwa na kuhojiwa kwa Askofu wa Kanisa la
Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye alikuwa rafiki yake na
‘muwezeshaji’ wake kabla siasa za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
hazijawageuza kuwa mahasimu.
Akizungumza
jana kanisani kwake wakati akiwasimulia waumini wake mkasa uliompata
tangu alipowasili katika kituo cha kati cha polisi jijini Dar es Salaam
hadi alipoachiwa, Askofu Gwajima alisema kuwa alipokea ujumbe wa Dk.
Slaa ambaye alimtetea dhidi ya tuhuma hizo.
Ujumbe wenyewe umewekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Askofu Gwajima na unasomeka hivi hapa chini
|
February 13, 2017
DKT.SLAA AMTUMIA UJUMBE GWAJIMA KUHUSU DAWA ZA KULEVYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment