Serikali wilayani Nyamagana
Mkoani Mwanza imetoa msaada wa vyakula kwa watu ambao nyumba zao ziliezuliwa paa na
mvua iliyonyesha wiki iliyopita iliyoambatana na upepo. Mvua hiyo
iliathiri kaya 231 zenye watu 800 ambao mpaka sasa hawana makazi.
Vyakula vilivyogawiwa ni kilo 3,760 za unga na kilo 1,000 za maharagwe
vyote vikiwa na thamani ya Sh7.3 milioni.
Akizungumza baada ya kukabidhi vyakula hivyo kwa nyakati tofauti, mkuu wa Wilaya ya Nyamagana,
Marry Tesha alisema msaada huo umetolewa na Serikali kwa kushirikiana na
wadau wengine.
Alisema vyakula katika Kata za Mahina waligawa kwa kaya
(94), Butimba (64), Nyegezi (61) na Mkuyuni (12). Mkuu huyo wa wilaya
aliwataka viongozi wa maeneo hayo kuhakikisha msaada huo unatumika kwa
malengo yaliyokusudiwa.
Pia, alito wito kwa wananchi kujenga nyumba imara
zinazoweza kuhimili mikikimikiki, kwa kuwa nyingi zilizobomoka, hazikuwa
imara.
Ally Juma, ofisa mtendaji wa Kata ya Mahina ambako nyumba za
kaya 94 ziliezuliwa, alisema wamiliki wameshindwa kupaua upya kutokana
na uduni wa kipato.
Ofisa Mtendaji Kata ya Nyegezi, Charles Musa alitoa
wito kwa wananchi kupanda miti kwenye makazi yao ili kuepuka madhara
yatokanayo na upepo mkali.
Naye Amina Rashid, ambaye ni muathirika wa
mvua hizo anayeishi Mahina, aliiomba Serikali iendelee kuwasaidia kwa
sababu madhara waliyoyapata ni makubwa na uwezo wengi ni mdogo.
|
February 6, 2017
MWANZA YATOA MSAADA WA CHAKULA KWA KAYA 231 ZILIZOATHIRIWA NA MVUA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment