KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

February 13, 2017

SEKTA YA UCHUKUZI KUELEKEA DODOMA

UKOP
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Leornard Chamuriho kabla ya kuwaaga watumishi wa Wizara hiyo  wanaohamia Dodoma leo, jijini Dar es salaam.
Picha na Biseko Ibrahim
…………
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewataka watumishi wa Wizara hiyo Sekta ya Uchukuzi kutumia vizuri fursa ya kuhamia Dodoma kwa kuwatumikia watanzania kwa uadilifu na weledi.
Amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akiwaaga watumishi wa Sekta ya uchukuzi wa awamu ya kwanza ambao wameondoka leo kuelekea mjini Dodoma.
“Nawapongeza kwa kupata fursa ya kuwa katika awamu ya kwanza katika Wizara hii kuhamia Dodoma fahamuni hii ni fursa na si changamoto kwani hatua hii inasogeza huduma karibu na wananchi hivyo watumikieni kwa moyo”, amesema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha watumishi wake wanahamia Dodoma na kuendelea na utekelezaji wa majukumu yake kwa wananchi.
Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho amesema awamu ya kwanza ya watumishi zaidi ya 45 inahamia Dodoma mwezi huu na Awamu ya pili itaanza mwezi wa Machi na watumishi wote wa sekta ya uchukuzi watakuwa Dodoma ifikapo Agosti mwaka huu.
“Watumishi wa Sekta ya Uchukuzi wanaohamia Dodoma katika awamu ya kwanza ni pamoja na Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi, Wakurugenzi na Wakurugenzi wasaidizi, wakuu wa vitengo na maafisa waandamizi”, amesisitiza Dkt. Chamuriho.
Stori na Biseko Ibrahim

No comments:

Post a Comment