TAREHE 06.02.2017 MAJIRA YA SAA
01:00HRS USIKU, KATIKA CHUO CHA UTAFITI WA SAMAKI NA UVUVI KILICHOPO
MTAA WA BUTIMBA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU WATANO
WANAOZANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAKIWA NA SILAHA ZA MAPANGA, VIPANDE CHA
NONDO NA WAKIWA WAMEVALIA MAKOTI MAREFU HUKU WAKIWA NA FUNGUO BANDIA
WALIVAMIA OFISI ZA CHUO TAJWA HAPO JUU NA KUJARIBU KUVUNJA OFISI KWA
LENGO LA KUPORA FEDHA, SAMAKI NA VITU MBALIMBALI VILIVYOMO NDANI,
POLISI WALIWAPA AMRI YA KUKAA CHINI YA ULINZI LAKINI WALIKAIDI NA KUANZA
KUKURUPUKA KUKIMBIA, NDIPO ASKARI WALIFYATUA RISASI KADHAA HEWANI HUKU
WAKIWAAMURU KUJISALIMISHA LAKINI WALIKAIDI AMRI HIYO, ASKARI
WALIWAFYATULIA RISASI ZA MIGUUNI ZILIZOWALENGA MAJAMBAZI WAWILI NA
KUFANIKIWA KUWAKAMATA AMBAO NI 1. RASHIDI SPAKI MIAKA 37, MUHA NA
MKAZI WA MKOLANI NA 2. ADAM MBALAMWEZI @ SAIDI MIAKA 38, MNYAMWEZI NA
MKAZI WA IGOGO, HUKU MAJAMBAZI WENGINE WATATU WAKIFANIKIWA KUTOROKA.
ASKARI WALIWACHUKUA MAJAMBAZI HAO
WALIOJERUHIWA KWA RISASI NA KUWAKIMBIZA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU
TOURE KWA AJILI YA MATIBABU ILI BAADAE WAKIPONA WAWEZE KUHOJIWA,
WATUHUMIWA WALIENDELEA KUPATIWA MATIBABU NA HALI ZAO ZILIKUWA
ZIKIENDELEA VIZURI LAKINI ILIPOFIKA MAJIRA YA SAA 5:00HRS ALFAJIRI YA
TAREHE TAJWA HAPO JUU, MTUHUMIWA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA RASHIDI SPAKI
ALIYEJERUHIWA KWA RISASI KWENYE PAJA/NYONGA JUU KUSHOTO ALIFARIKI
DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU, AIDHA MWENZAKE AITWAYE ADAM
MBALAMWEZI ALIYEPATA JERAHA KWENYE MGUU WA KUSHOTO ALIKUWA AKIENDELEA
VIZURI NA TAYARI AMERUHUSIWA HOSPITALI YUPO POLISI KWA MAHOJIANO ZAIDI.
AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA
KUTOKA KWA RAIA WEMA JUU YA UWEPO WA WATU MAJAMBAZI AMBAO WAMEPANGA
KUVAMIA OFISI TAJWA HAPO JUU WAKIWA NA SILAHA NDIPO UFUATILIAJI WA
HARAKA JUU YA TAARIFA HIZO ULIFANYIKA, ASKARI WALIFIKA MAPEMA ENEO LA
TUKIO NA KUWEKA MTEGO WA KUWAKATA MAJAMBAIZI HAO, GHAFLA MAJAMBAZI
WATANO WALIFIKA ENEO LA TUKIO WAKIWA WAMEVALIA MAKOTI MAREFU WAKIWA
KATIKA HARAKATI ZA KUVUNJA OFISI NA KUPORA. POLISI WALIWAZINGIRA
MAJAMBAZI HAO NA KUWAPA AMRI YA KUKAA CHINI YA ULINZI LAKINI WALIKAIDI
NA KUKURUPUKA NA KUANZA KUKIMBIA NDIPO ASKARI WALIFYATUA RISASI KADHAA
HEWANI HUKU WAKIWAAMURU MAJAMBAZI HAO KUJISALIMISHA LAKINI WALIENDELEA
KUKAIDI AMRI HIYO, NDIPO ASKARI WALIWAFYATULIA RISASI ZA MIGUUNI
ZILIZOWALENGA MAJAMBAZI WAWILI TAJWA HAPO JUU, HUKU MAJAMBAZI WENGINE
WATATU WAKIFANIKIWA KUTOROKA.
KATIKA TUKIO HILO ASKARI WALIWEZA
KUKAMATA MAPANGA MAWILI, NONDO, TUPA NA FUNGUO BANDIA AMBAZO ZILIKUTWA
KWENYE SURUALI ALIYOVAA MAREHEMU BAADA YA KUFANYIWA UPEKUZI. WATUHUMIWA
WALIOKAMATWA WALIPOHOJIWA WALIKIRI TUHUMA ZA KUHUSIKA KATIKA MATUKIO
KADHAA YA UHALIFU YALIYOTOKEA HAPA JIJINI MWANZA, AIDHA WALIKIRI TUHUMA
ZA SKUHUSIKA KWENYE TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA LILILOTOKEA
KATIKA GHALA LA KIWANDA CHA VICK FISH KILICHOPO IGOGO WILAYA YA
NYAMAGANA AMBAPO MAJAMBAZI HAO WALIVUNJA NA KUPORA MABONDO YA SAMAKI
YENYE THAMANI YA TSH 150,449,400/=, AMBAPO ILIFUNGULIWA KESI YENYE KUMBU
NAMBA MWS/IR/439/2016.
AIDHA WALIKIRI PIA TUHUMA ZA
KUHUSIKA KATIKA TUKIO LA MARA YA PILI KWENYE KIWANDA HICHOHICHO CHA VICK
FISH KILICHOPO IGOGO AMBAPO WALIVUNJA USIKU LAKINI HAWAKUFANIKIWA
KUPORA KITU CHOCHOTE KWANI WAKATI WAKIWA KWENYE JITIHADA ZA KUTOA
MABONDO YA SAMAKI POLISI WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA MAJAMBAZI HAO
WALIKIMBIA, AMBAPO ILIFUNGULIWA KESI YENYE KUMBU NAMBA MWS/1R/5807/2016,
YA KOSA YA KUVUNJA GHALA USIKU KWA NIA YA KUIBA.
POLISI WANAENDELEA NA MAHOJIANO
NA MTUHUMIWA AMBAYE ANAENDELEA KUSHIKILIWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA
ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, UPELELEZI NA MISAKO JUU YA WATUHUMIWA WENGINE
WATATU AMBAO WALIFANIKIWA KUTOROKA UNAENDELEA ILI WAKAMATWE PIA WATOE
SILAHA AMBAYO WANAYO, MWILI WA MAREHEMU UPO HOSPITALI YA RUFAA YA
BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA RAI KWA WAKAZI WA JIJI NA
MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA TAARIFA POLISI ZA WAHALIFU NA
UHALIFU MAPEMA, ILI KUWEZA KUZUIA LAKINI PIA ILI WAWEZWE KUKAMATWA NA
KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA. AIDHA ANAWASIHI VIJANA KUFANYA KAZI
ZILIZO HALALI ILI WAJIEPUSHE NA MATATIZO AMBAYO YANAWEZA KUGHARIMU
MAISHA YAO.
IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
|
February 7, 2017
TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment