Mkuu wa kitengo cha Watoto wenye ulemavu wa akili katika shule ya Uhuru Mchanganyiko,Eugen Stephano, (kulia) akipokea msaada wa vifaa vya shule kutoka Wafanyakazi wa Kampuni ya TBL Group |
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakifurahi na wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia katika shule ya msingi Msasaani jijini Dar es Ssalaam, kitengo cha viziwi wakati wa maadhimisho ya siku ya wapendanao . |
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mwanza wakiangalia watoto wenye ulemavu wanavyofundishwa katika kituo cha Huruma jijini Mwanza |
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakifundisha watoto kusoma katika shule ya Msasani |
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group katika picha ya pamoja na watoto wenye ulemavu wanaosoma katika shule ya Msasani.
…………………
Wafanyakazi
wa kampuni ya TBL Group wameitumia siku ya Wapendanao kusaidia na kutoa
faraja kwa watoto wanaosoma kwenye shule za walemavu katika mikoa ya
Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya,Kilimanjaro na Arusha ambapo pia walitoa
misaada ya kufanikisha masomo kwa wanafunzi hao.
Kwa kutumia kauli mbiu ya Sambaza upendo,Sambaza furaha
wameweza kutekeleza moja ya mkakati wa kampuni kuhudumia jamii
kukabiliana na changamoto mbalimbali katika maeneo inakofanyia biashara
zake ikiwemo kuhamasisha wafanyakazi wake kutumia muda katika shughuli
mbalimbali za kijamii.
Meneja Mawasiliano wa TBL Group,Amanda Walter,ameeleza kuwa wameamua kuitumia siku hii kusambaza upendo na furaha kwa watoto wa shule zenye wanafunzi wenye ulemavu ambapo wafanyakazi wamezitembelea na kushiriki shughuli mbalimbali katika maeneo hayo ikiwemo kucheza na kutoa zawadi kwa watoto kwa ajili ya kuwapatia faraja.
“Mkakati
wetu zaidi katika kusaidia changamoto zilizopo kwenye jamii haulengi
kutoa fedha na zawadi bali wafanyakazi kujitoa muda wao kushiriki katika kazi
za jamii kama vile kusafisha mazingira,kufundisha watoto.kupaka rangi
majengo ya shule,kupanda miti ,kuwatembelea wagonjwa ,kusafisha maeneo
ya hospitali na tumekuwa mstari wa mbele pia kushiriki matembezi
mbalimbali ya hisani yenye lengo la kuchangia kuondoa changamoto za
kijamii”.Alisema Amanda.
Alisema
TBL Group itaendelea kushiriki shughuli za kijamii kwa kuwa moja ya
sera yake ni kuwaleta watu pamoja na kufanya maisha yao kuwa murua
inaelekeza kusaidia jamii na kuleta maendeleo endelevu kwa jamii kupitia
biashara zake. “Kampuni imekuwa mstari wa mbele kusaidia kukabiliana na
changamoto mbalimbali hususani katika sekta ya elimu,afya na maji ,uwezeshaji wanawake kiuchumi na kampeni za usalama barabarabani.
Mkurugenzi
wa Kituo cha watoto wenye ulemavu Huruma Special Unit, Andrew Jacob
ameishukuru kampuni ya TBL Group na wafanyakazi wake kwa kuwakumbuka
watoto wenye
mahitaji maalumu hususani katika kuadhimisha siku ya wapendanao,”Kwa
niaba ya shule nawashukuru na mmedhihirisha upendo wa kweli kwa
kuwakumbuka watoto hawa na kushirikin kucheza nao na kuwapatia zawadi na
faraja ya upendo”.Alisema.
|
No comments:
Post a Comment