KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

February 13, 2017

UTAMADUNI WA MTANZANIA NI SEHEMU YA KIVUTIO CHA UTALII: WAZIRI NAPE

NP2
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla akizungumza wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
NP5
Baadhi ya Wasanii kutoka Iran wakitumbuiza muziki wa Ala wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
NP7
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akisikiliza maelezo kuhusu michoro ya Kiutamaduni ya Iran wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
NP10
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akipiga Gitaa  lililotengenezwa na Msaanii wa Uchoraji na Uchongaji Bw. Washington Steven Masanja (kushoto) wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam.Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
NP12
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng akimkabidhi zawadi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye  wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.
NP13
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akifurahia jambo na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.
NP14
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng na baadhi ya viongozi kutoka taasisi za Serikali na ubalozi wa Iran wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana. 
Picha na: Frank Shija – MAELEZO.
…………………………………………………………
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
 Serikali chini ya Wizara ya Hbari Utamaduni Sanaa na Michezo inaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa Utamaduni wa Mtanzania unakuwa sehemu ya muhimu ya kivutio cha Utalii ili kutengeneza ajira na kuingizia Serikali mapato.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye alipokuwa anafungwa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa madhimisho haya yanaimarisha undugu wa damu wa kiuchumi na kiutamaduni ulioachwa na wahenga.
“Maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Shirazi ni fursa pekee ya kujifunza kutoka kwa kwa wairani namna ya kukuza ,kulinda na kuendeleza Utamaduni,Sanaa,Filamu,Mila na Desturi zetu”Alisema Waziri Nape.
Aidha ameongeza kuwa Wizara yake  itaweza kufanikisha shughuli za Utamaduni na kuziendeleza  kwa kushirikiana na wadau  wa ndani na nje ya ya nchi  kama ilivyofanyika katika maadhimisho ya mwaka huu kwani yanatangaza vikundi vya Sanaa na Wasanii.
Kwa upande wa wake Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Irani hapa nchini Bw.Ally Baghari amesema kuwa ushirikiano wa Kiutamaduni baina ya Tanzania na Irani umeongeza mafanikio ya kiuchumi na kijamii katika nchi hizo hasa kupitia ubadilishanaji wa Utamaduni tangu enzi za ukoloni.
“Tumejifunza utamaduni  wa kitanzania kupitia maadhimisho haya na tunaamini watanzania pia wamejifunza utamaduni wa Irani ambao umesaidia kuimarisha ushirikiano wetu”Alisema Bw Baghari.
Maadhimisho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.

No comments:

Post a Comment