Taarifa
zinadai kuwa mrembo Agnes ‘Masogange’ Gerald amekamatwa na polisi usiku
wa kumkia leo, ikiwa ni sehemu ya msako wa watu wanaohusishwa na
biashara ya dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa Jamii Forums, Masogange anashikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam.
Mrembo huyo anakuwa staa mpya kuingizwa kwenye orodha ya mastaa wengine waliohusiswa na sakata hilo.
Kwenye
mazungumzo yaliyovuja hivi karibuni na kusambaa mtandaoni, Wema Sepetu
aliyekuwa ameshikiliwa pia kituoni hapo kwa sakata kama hilo, alisikika
akimtaja Masogange kuwa mmoja wa mastaa wanaoshukiwa kujihusisha kwenye
biashara hiyo.
Hiyo
sio mara ya kwanza kwa Masogange kushikiliwa na polisi kwa tuhuma hizo.
August 2014, Kikosi Kazi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya nchini
kilimhoji kwa zaidi ya saa 10 mrembo huyo kuhusiana na tuhuma za
kukamatwa na dawa aina ya crystal methamphetamine huko Afrika Kusini,
Julai mwaka 2014.
Masogange
alitawala vyombo mbalimbali vya habari nchini mwaka 2014 baada ya
kukamatwa Afrika Kusini akiwa na nduguye Melisa Edward wakiwa na ‘mzigo’
wa dawa hizo zenye thamani zaidi ya Sh6.8 bilioni.
Wasichana hao walinaswa baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Katika mahojiano hayo, Masogange alidai kuwa alipewa dawa hizo na mtu ambaye hamfahamu kwa jina lakini anaikumbuka sura yake.
|
February 15, 2017
VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA:MASOGANGE ADAIWA KUKAMATWA NA POLISI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment