. Mkazi wa Nyasaka mkoani Mwanza Michael Alfred,
akipokea simu
aina ya Smart Bomba ikiwa ni zawadi kutoka kwa Mkuu wa Vodacom
Tanzania Kanda ya ziwa ,Ayubu Kalufya,baada ya kununua moja ya simu hizo wakati wa kuzitambulisha
simu hizo jijini Mwanza.
Wakazi
wa jiji la Mwanza wamezifurahia simu za kisasa za Smart Bomba ambazo
zilizinduliwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania hivi
karibuni,Simu hizo zinazidi
kuchangamkiwa na wananchi wengi hususani wakazi wa maeneo ya jiji la
Mwanza na wanaozunguka mkoa huo ambapo wameshukuru kwa hatua hiyo ambayo
imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya mawasiliano nchini.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti wakati wa promosheni ya mauzo ya simu hizo
inayoendelea mkoani Mwanza,baadhi ya wananchi wamesema kuwa hatua ya
kampuni hiyo kuingiza sokoni
simu za kisasa za Smart Bomba zinazopatikana kwa gharama nafuu
imedhihirisha dhamira ya kweli ya kampuni hiyo ya kuwapeleka watanzania
katika ulimwengu wa kidijitali.
Bw.Focus
Phabian mmoja wa wananchi ambaye amenunua simu hiyo akiongea kwa niaba
ya wenzake alisema kuwa Smart Phone ni mkombozi wa mawasiliano ya kisasa
kwa kuwa licha ya
kuwa na unafuu wa bei pia imetengenezwa kwa kuendana sambamba na
mazingira halisi ya watanzania.
“Simu
ya Smart Bomba licha ya kuuzwa kwa shilingi 99,000 ambazo ni nafuu kwa
watanzania wengi programu zake zinapatikana katika lugha ya taifa ya
Kiswahili bila kusahau
muundo wake unaowezesha kupata interneti yenye kasi kubwa ya Vodacom na
kupiga picha zenye ubora wa hali ya juu .”Alisema.
“Watanzania
wengi hivi sasa wana kiu ya kupata taarifa mbalimbali zinazotokea papo
kwa papo na kujiunga pia na progamu za simu zinazorahisisha mawasliano
kama whasap hivyo
kwa Smart Bomba wengi watamudu kutumia simu za kisasa za intanenti
ambazo zinauzwa kwa bei nafuu na zilizotengenezwa kwa kulenga mazingira
halisi ya kitanzania”,Alisema Phabian.
Mkuu
wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,kanda ya ziwa,Ayoub
Kalufya,alisema kuwa tangu simu hizi ziingizwe sokoni wiki moja
iliyopita kumekuwepo na mwitikio mzuri
wa wananchi ambao wamekuwa wakizinunua ili kuingia katika ulimwengu wa
kidigitali.
“Smart
Phone mbali na kuwa na unafuu wa bei pia inaambatana na ofa ya mteja
anayenunua simu kuunganishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 10 za
bure kwa mwezi na ofa
hii inatolewa katika kipindi cha miezi 3 mfululizo kwa ajili ya
kumuwezesha mteja kupata na kufurahia intanenti i yenye kasi kubwa ya
Vodacom mahali popote na wakati wowote”,Alisema Kalufya.
Kalufya
aliongeza “wakati ni huu kwa wakazi wa jiji la Mwanza mikoa mingine ya
kanda ya ziwa makundi kuchangamkia fursa hii pekee kwa kununua simu ya
Smart Bomba kwa gharama
nafuu na kufurahia mawasiliano ya kisasa”.
|
No comments:
Post a Comment