Mama wa mtoto huyo, Julieth Daudi
Na Dotto Mwaibale
SAKATA la
Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini pamoja na ndugu zake kususia
kuchukua mwili wa mtoto aliyejifungua kwa madai kuwa mtoto huyo hakuwa
wake baada ya kubadilishiwa na wauguzi wa Hospitali ya Amana katika
Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam baada ya kujifungua limechua
sura mpya kufuatia wazazi hao kutaka kwenda kumuona Waziri wa Afya kufikisha kilio chao.
Akizungumza
na Jambo Leo nyumbani kwao Dar es Salaam jana, Daudi alisema
tunahitaji kwenda kumuona Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na
Watoto, Ummy Mwalimu kwa hatua zaidi kutokana na kitendo hicho walichofanyiwa na wauuguzi hao.
“Mimi pamoja na ndugu zangu tutakwenda kumuona waziri ili kumpelekea malalamiko yetu” alisema Daudi.
Akizungumzia
mkasa huo Daudi alisema alifika Hospitalini hapo Februari 2 jioni
akiwa amesindikizwa na mama yake Veronica Lucas na shangazi yake Judith
Christopher.
“Nilipofika
daktari aliponipima aliniambia kuwa hasikii mapigo ya mtoto isipokuwa
ya kwangu hivyo alishauri siku iliyofuata nipate kipimo cha utrasaund
lakini kabla ya
kipimo hicho nilijisia uchungu na kujifungua” alisema Daudi.
Daudi
alisema baada ya kupita muda kidogo muuguzi aliyemzalisha alimfuata na
kumueleza kuwa mtoto wake alikuwa amefariki na alipomuuliza alikuwa wa
jinsia
gani muuguzi huyo alimweleza kuwa alikuwa hajui kama alikuwa wa kiume au wa kike.
Aliongeza
kuwa wakati yupo wodini alimuona kijana mmoja aliyevalia koti la
hospitali akiwa amembeba mtoto ambaye hakujua alikokuwa amempeleka.
Alisema
baada ya kuambiwa mtoto wake amefariki aliomba aonyeshwe lakini
hakuoneshwa tangu saa tatu asubuhi ambapo alilazimika kwenda kuomba
simu kwa mlinzi wa hospitali hiyo na kuwajulisha ndugu zake walipofika nao waliomba kuonyeshwa mwili wa mtoto huyo bila mafanikio.
Shangazi
wa Julieth Judith Christopher alisema baada ya kutokea tukio hilo
walikwenda kumuona Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye aliitisha kikao
baina
ya ndugu
pamoja na maofisa wengine wa hospitali hiyo ambacho hakikufikia muafaka
baada ya ndugu hao kukataa kuuchukua mwili wa mtoto huyo wakidai si wa
kwao.
Aliongeza
kuwa mganga mkuu huyo aliwaeleza kuwa mtoto huyo alikuwa amefia tumboni
baada ya mimba hiyo kuharibika na ndiyo sababu mtoto huyo alizaliwa
akiwa
mfu.
“Wanafamilia tumegoma kuuchukua mwili wa mtoto huyo na maamuzi yaliyofikiwa ni kufanyika kipimo cha DNA” alisema Christopher.
Alipopigiwa simu Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Beauty Mwambebule alisema hawezi kulizungumzia tukio hilo kwenye simu njia ya simu badala yake alimtaka mwandishi wetu kwenda hospitali kupata undani wa jambo hilo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062) |
February 6, 2017
WALIOGOMEA MAITI HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR ES SALAAM KWENDA KWA WAZIRI WA AFYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment