Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau Redio na vyombo
vya habari kwa ujumla katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani
yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amevishauri vyombo vya habari nchini
kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph
Pombe Magufuli katika vita dhidi ya madawa ya kulevya nchini.
Ameyasema hayo wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliofanyika katika Chuo Kikuu
huria cha Tanzania na kusisitiza kuwa vyombo vya habari viwe sehemu ya
kuwaunganisha watanzania katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.
“Wanahabari tuliunganishe taifa letu tuwe kitu kimoja katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya” alisisitiza Mhe. Nnauye.
Ameongeza kuwa sasa ni wakati wa
watu wote kuungana kwa pamoja zikiwemo tasnia zilizopo katika Wizara
yake za Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwani vita hii ni ya
watanzania wote na sio mtu mmoja au Serikali pekee.
Aidha Mhe. Nape amevitaka vyombo
vya habari kutobaki nyuma katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya na
kuhakikisha haki inatendeka na vita dhodi ya madawa ya kulevya
vinashinda.
|
February 14, 2017
WANAHABARI TUMUUNGE MKONO RAIS KATIKA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment