Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza na Wanahabari kuhusu Wizara yake
ilivyotekeleza Agizo la Rais Dkt. John Magufu kuhusu kumlipa Mkandarasi ayejenga Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3).
Kwa mujibu wa
Katibu Mkuu Doto James, Wizara ya Fedha na Mipango imemlipa Mkandarasi
anayejenga Mradi wa upanuzi wa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere(Terminal 3) Kampuni ya BAM International kiasi cha Euro Milioni 9.5
sawa na zaidi ya Tsh. Bilioni 22 za
Kitanzania mara baada ya kuhakiki madai hayo.
Katika Hatua
nyingine Wizara ya Fedha inaandaa Malipo ya awali (Advance Payment) kiasi cha
Tsh. Bilioni 300 kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi anayejenga Mradi wa Ujenzi wa
Reli ya Kisasa ya Kutumia Umeme na Mafuta(Standard Gauge) katika awamu ya
kwanza itakayoanzia kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro katika awamu yake ya
kwanza ya Ujenzi huo. (PICHA NA MPIGA PICHA WETU)
No comments:
Post a Comment