Na.Alex Mathias
Mabingwa Watetezi wa Comoro timu
ya Ngaya FC imeanza vibaya katika Michuano ya awali ya Kombe la Ligi ya
Mabingwa barani Ulaya baada ya kukubali kichapo cha Paka Mwizi toka kwa
Mabingwa wa kihistoria nchini Tanzania Yanga cha jumla ya Magoli 5-1 na
kujiweka katika nafasi finyu ya kusonga mbele.
Mchezo ulianza kwa kasi huku wachezaji wa Ngaya wakiwa na maumbo makubwa na Warefu waliwapa shida vijana wa Kocha wa Yanga Lwandamina huku washambuliaji wa Yanga wakikosa nafasi nyingi za wazi na kama wangekuwa makini wangeondoka na magoli mengi.
Dakika ya 43 kiungo mkabaji toka Zambia Justine Zullu alifunga bao la kwanza baada ya kupokea pasi toka kwa Obrey Chirwa na Simon Msuva alifunga la pili dakika ya 45 kwa shuti la Mita 18 ambalo lilimshinda Mlinda Mlango wa Ngaya Said Komandoo hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa magoli mawili.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu
zote kufanya mabadiliko hata hivyo wanajangwani waliweza kutumia nafasi
ambazo waliweza kuzipata Obrey Chirwa
alifunga la tatu dakika ya 59 baada ya Kamusoko kupigia pande la pasi
na dakika ya 65 Mshambuliaji mwenye rekodi ya Tuzo Tanzania Amis Tambwe alifunga la nne akipokea krosi toka kwa beki Juma Abdul.
Akitokea benchi Said Khalfan
aliifungia Ngaya bao la kufutia machozi baada ya kuwazidi ujanja mabeki
wa Yanga dakika ya 66 hata hivyo furaha yao haikuweza kudumu kwani
dakika ya 73 Juma Mahadhi alipigilia msumari wa tano kwa pasi safi toka
kwa Thabani Kamusoko.
Hadi mwamuzi anamaliza Mpira Yanga
wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli 5-1 na kujiweka katika nafasi
nzuri ya kusonga mbele hatua inayofuata na timu hizo zinatarajia
kurudiana Februari 18 jijini Dar es salaam huku Ngaya wanatakiwa
kushinda jumla ya magoli 6-0 ili waweze kusonga mbele na endapo Yanga
watasonga mbele watakutana na APR ya Rwanda au Zanaco ya Zambia ambazo
jana ziliweza kutoka sare ya bila kufungana na Yanga wanatarajia kurudi
siku ya Jumanne na kujiandaa na mchezo wa marudiano.
No comments:
Post a Comment