Jeshi
la Polisi nchini Kenya limepoteza Askari wake watano baada ya gari lao
kukanyaga bomu lililotegwa barabarani katika mji wa Liboi karibu na
mpaka na Somalia.
Polisi
hao wameuawa na shambulio lililotokea katika eneo ambalo Polisi wengine
wanne waliuawa katika shambulio kama hilo lililotekelezwa na kundi la
Alshabab hivi karibuni.
Wapiganaji
wa kundi la Al-Shabab ambao makao yao makuu ni Somali, wameendelea
kufanya mashambulio kadhaa nchini Kenya katika siku za hivi karibuni,
wakiitaka Serikari ya Kenya kuondoa majeshi yake yanayofanya kazi katika
vikosi vya AMISOM.
No comments:
Post a Comment