==>
Mwanamuziki,Diamond Plantinumz alikuwa nchini Kenya kwa ajili ya
tamasha la Koroga ambalo lilifanyika jana Jumapili Mei 28
==>
Diamond aliwahutubia wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi na kuzungumzia
kifo cha aliyekuwa mme wa mkewe wa sasa, Ivan Ssemwanga
==> Ssemwanga alifariki akiwa amelazwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini baada ya kukumbwa na mshtuko wa moyo
****
Mwanamuziki,
Diamond Plantinumz amezungumzia kifo cha aliyekuwa mme wa mkewe ,Zari
Hassan ambaye alifariki juma lililopita akipokea matibabu katika
hospitali moja Afrika kusini.
Akizungumza
akiwa katika chuo kikuu cha Nairobi Ijumaa Mei 26, Diamond alisema kuwa
Zari anapitia wakati mgumu ikizingatiwa kuwa alizaa watoto watatu na
Ssemwanga .
Aidha
,Diamond alisema kuwa hangekosa kwenda Kenya kuhudhuria tamasha la
Koroga kwa sababu alikuwa tayari amewaahidi Wakenya kwamba angeenda
kabla ya msiba huo kutokea.
Diamond alisema atahudhuria mazishi ya mwenzake,Ssemwanga.
"Kwa
kweli umekuwa ni wakati mgumu kufutilia mbali mualiko huu. Nimeongea na
mke wangu akanielewa. Nikimaliza hapa nitaenda Uganda kwa sababu ya
mazishi," Diamond alisema.
No comments:
Post a Comment