Mshambuliaji wa timu ya Azam FC ,John Bocco ni mali ya Simba,. Taarifa zinaeleza amesaini miaka miwili katika kikosi cha Simba.
Taarifa zinaeleza
mkataba huo ni wa awali na inaonekana Bocco ameamua kutua Simba baada ya
makubaliano yake na Azam baada ya mkataba wake kwisha, kuonekana
unakwenda kombo.
Hata hivyo, Bocco amekuwa hapokei simu ili kulithibitisha
hilo suala ingawa hivi karibuni alikanusha kila kilichoandikwa kwenye
akaunti yake ya Instagram kuhusiana na kwamba ana mpango wa kuondoka
Azam.
Alidai akaunti yake ilikuwa imetekwa lakini hali halisi ilionyesha kwamba hakuwa amezungumza lolote.
Afisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddi yeye alisema walikuwa katika mazungumzo na Bocco baada ya mkataba wake kufikia tamati.

No comments:
Post a Comment