Na Seleiman Ussi Zanzibar .
ZFA Taifa Pemba imeiteremsha
daraja timu ya Maji Maji kutoka ligi kuu ya Zanzibar, hadi daraja la
kwanza Taifa msimu wa 2017/2018, pamoja na kuitoza faini ya shilingi
Milioni 1,200,000/= kwa makosa mawili tafauti.
Kosa la kwanza kwa Timu hiyo
katika mchezo wake na Shaba wa Aprili 28 mwaka huu, timu ya Maji Maji
ilifika Uwanjani na wachezaji nane tu na kupekea baadhi ya wachezaji
kuanguka uwanjani na kushindwa kuendelea
na mchezo huo.
Kaimu Msaidizi Katibu Mkuu ZFA
Taifa Khamis Hamad Juma, alisema baada ya hali hiyo mwamuzi wa mchezo
huo alilazimika kulivunja pambano hilo
dakika ya 44, huku Shaba ikiwa inaongoza kwa goli 1-0.
“Kutokana na hali ilivyokuwa
uwanjani baada ya wachezaji watatu kuumia, wakabakia wachezaji watano
mwamuzi hakuweza kuendelea na mchezo na kulivuanja pambano”. Alisema.
Alisema kwa mujibu wa kanuni za
kuendeshea mashindano ya Mpira wa Miguu Zanzibar, Kifungu namba 21
(a)(i) timu ya Maji Maji imepoteza mchezo huo na shaba kuwepwa ushindi,
pamoja na kuteremshwa daraja la kwanza Taifa kwa msimu 2017/2018 na
kutozwa faini ya laki 600,000/= faini ambayo inatakiwa kulipwa Mei 30
mwaka huu.
Khamis alisema kosa la pili kwa
timu hiyo katika mchezo wake na Jamhuri wa Aprili 26 mwaka huu katika
uwanja wa FFU Finya, ulishindwa kumalizika kwa wakati baada ya wachezaji
Abrahman Haji Othaman, Bakar Said Ginyari, Branka Ali Yassin jezi,na
Ibrahim Said Juma kumpiga mwamuzi.
No comments:
Post a Comment