Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji amejiuzulu wadhifa huo akidai kuwa anatoa nafasi kwa watu wengine kuiongoza.
Kupitia barua yake, Manji amesema kuwa anaondoka akiamini ameiacha Yanga ikiwa timu yenye mafanikio kisoka nchini.
"Muda
wangu wa kutangaza kuwa ninakaa pembeni kutoka kwenye nafasi ya
uenyekiti ni sasa. Tayari tumekuwa mabingwa watetezi mashindano tena
tuna kizuri cha wachezaji na makocha. Tumeungana kwa pamoja haijawahi
kutokea, " imesema sehemu ya barua hiyo.
Akizungumza kwenye kipindi cha Sports Headquarters kinachoendeshwa na kituo cha radio cha EFM, Manji amekiri kujiuzulu.
"Hiyo taarifa ni sahihi na sababu za kujiuzulu zipo humo, " amejibu Manji kwa kifupi.
Kwa
mujibu wa barua ya Manji iliyoisaini Mei 22, inasema amejiuzuru
uenyekiti na sasa majukumu yote hadi pale uchaguzi mpya utakapofanyika
wa kujaza nafasi yake majukumu yote ya timu yatakuwa chini ya Makamu wa
Rais, Sanga.
Sanga
alithibisha kupokea barua ya Manji kujizuru akisema ni kweli nimepokea
barua ya mwenyekiti juu ya uamuzi wake wa kupumzika kwa sasa.
Katika
barua Manji aliisema huwa kunafika muda tukiwa tunafuata wito fulani,
wakati mimi nikiwa sehemu ya Yanga ilinibidi nijitokeze mbele kwa ajili
ya umoja wa klabu yetu tuipendayo na kuongoza. Kulikuwa na wanachama
waliokuwa wakigombana, ndipo ilikuwa muda wangu wa kutoa msaada kwa
Yanga.
"Sisi
sote ni sehemu ya ukoo mkubwa wa Yanga na ukweli mnaufahamu, imani
ndiyo jambo ambalo tulilihitaji ndani ya Yanga kuturudisha katika
mwelekeo sahihi wa miaka 11 iliyopita."
Taarifa
hiyo iliendelea kusema "Kama Mungu alivyotuonyesha kwa kubadili jiwe
kuwa mkata, hivyo msaada wangu kwa uwezo wa neema zake, naamini ulifanya
mabadiliko chanya na klabu iko imara na huru. Lakini umefikia wakati
wangu wa kuachia wengine na wengeni wasifikirie nilikuwa kiongozi
aliyetaka cheo chochote au umashuhuri, ila ni upendo uliomgusa
kuitumikia Yanga yetu. Pamoja tulifanikiwa mengi sana, na kuandika
historia ndani ya Yanga na nilipolea baraka zenu mimi binafsi na familia
yanga kupitia furaha japo ndogo, iliyoweza kuwaletea, ambao
ninawashukuru sana.
"Nilisema
tangu mwaka 2014, kuwa sitagombea katika uchaguzi wa uongozi kwenye
nafasi yoyote ndani ya klabu na nikaonyesha mfano kuwa klabu yetu siyo
mtu mmoja ila ni yetu sote, na uongozi ni lazima utoke kutoka kwenye
kizazi kimoja kwenda kingine.
Iliongeza
taarifa hiyo kuwa "Lakini mwaka jana tulikuwa katika mashindano ya
mabara na kuacha pengo isingekuwa sahihi, hivyo kinyume na msimamo wangu
niligombea uenyekiti wa Yanga na kupata ushindi bila ya kupigwa, lakini
kama nikiendelea, nitakuwa ninaonyesha mfano upi kwa watoto wetu ambao
wanaipenda Yanga kwa sababu yetu? Kwani Yanga siyo klabu yao kama
ilivyokuwa yenu na mimi?"
Muda
wangu wa kutangaza kuwa ninakaa pembeni kutoka kwenye nafasi ya
mwenyekiti wa Yanga ni sasa, tayari tumekuwa mabingwa wa mashindano
tena, tuna kikosi kizuri na wachezaji na makocha, tumeungana kwa umoja
haijawahi kutokea, tumerudisha heshima ya kuwa washindano wa ukweli
katika klabu Afrika, na kuwa imara zaidi kiuchumi na mkataba wa
ufadhili ya Sportspesa.
Nafahamukuwa
bado kuna mengi yanayohitajika kutimizwa, lakini barabar ya mambo
yanayotakiwa kutimizwa haiwezi kuisha, na siwezi kuwa mroho wa kuamini
kuwa ni mimi pekee nitakayeweza kutufikisha mwisho wa safari.
Muda
wangu kama mwenyekiti wa klabu yetu ulikuwa umeongezwa tu na
haikumaanisha katika demokrasi yetu uwe ni ule usiokuwa na kikomo.
No comments:
Post a Comment