![]() |
Ufyatulianaji mkali wa risasi
umezuka katika miji miwili mikuu nchini Ivory Coast, wanajeshi
wakiendelea kuasi kwa siku ya nne mtawalia.
Wanajeshi hao
waliogoma wamefunga barabara nje ya kambi za jeshi katika mtaa wa
kifahari Abidjan, mji mkuu wa kibiashara wa Ivory Coast, mwandishi wa
BBC mjini humo anasema.Wanajeshi watiifu kwa serikali wameelekea katika mji wa pili, Bouaké, ambapo ufyatulianaji wa risasi pia umesikika. Mkuu wa majeshi ya nchi hiyo Jenerali Sékou Touré ameapa kumaliza maasi hayo, ambayo yalitokana na mzozo kuhusu malipo. Kupitia taarifa Jumapili, Jenerali Touré alisema wengi wa wamnajeshi hao waliogoma walikuwa awali wameitikia wito wa kuwataka wasitishe mgomo wao. Lakini operesheni ya kijeshi imeanzishwa kwa sababu baadhi ya wanajeshi wameendelea kupuuza maagizo ya wakuu wao, amesema. Wanajeshi hao waasi wameapa kujibu mashambulio iwapo watakabiliwa na wanajeshi watiifu kwa serikali. Milio ya risasi imesikika katika kambi ya jeshi ya Akouédo, mtaa ambao huwa na wakazi wengi wa mapato ya wastani nchini Ivory Coast na ambapo pia raia wa kigeni hupenda sana kuishi, mwandishi wa BBC aliyepo Abidjan Tamasin Ford anasema. |
May 15, 2017
MILIO YA RISASI YATANDA MJI MKUU WA IVORY COST
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment