KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 17, 2017

TAIFA STARS YAPANGWA NA MALAWI, ANGOLA COSAFA 2017

Na Mahmoud Zubeiry, LIBREVILLE
TANZANIA imepangwa Kundi A pamoja na Mauritius, Malawi na Angola katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika, COSAFA Castle 2017 inayotarajiwa kufanyika Afrika Kusini kuanzia Juni 25 hadi Julai 9, mwaka huu.
Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online mjini hapa leo, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema kwamba droo ya COSAFA imepangwa leo Afrika Kusini na wameangukia Kundi A.
“Na tukifanikiwa kuongoza Kundi A, tutamenyana na mabingwa watetezi, Bafana Bafana katika Robo Fainali,”amesema Malinzi ambaye yupo hapa Gabon na timu ya taifa yta vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys inayoshiriki Fainali za Afrika.
Taifa Stars inashiriki kama mgeni mwalikwa kwenye michuano hii kwa mara ya tatu baada ya mwaka 1997 na 2015, huku kisiwa cha Comoro kikithibitisha kushiriki mwaka huu.
Swaziland itamenyana na kinara wa Kundi B, linaloundwa na Zimbabwe, Madagascar, Msumbiji na Shelisheli.
Robo Fainali nyinginr mbili itazikutanisha Botswana na Zambia na washindi wa mwaka 2015, Namibia watamenyana na Lesotho.
Michuano hiyo ilifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1997 na kila nchi baina ya Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe imeshinda taji hilo mara nne, huku Angola imeshinda mataji matatu na Namibia moja.

No comments:

Post a Comment