Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia akisoma
hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo wakati wa ufunguzi wa
warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na
namna ya kuitekeleza inayoendelea katika ukumbi wa MUHAS jijini Dar Es
Salaam.WATU waliopembezoni ambao wamekuwa na shida kubwa ya kupata madaktari
bingwa, wataanza kupata nafuu baada ya kuanza kwa mradi wa tiba mtandao
unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi-Muhimbili, UNESCO pamoja na wadau wengine. Hayo yalisemwa katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza. Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Zulmira Rodrigues utoaji huo wa tiba mtandao kwa majaribio utaanza mapema zaidi kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu. |
May 17, 2017
TIBA MTANDAO KUANZIA OLOLOSOKWAN OKTOBA MWAKA HUU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment