Na Tiganya Vincent, Sikonge
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ameteua timu ya Maafisa watano wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa ajili ya kuandaa taarifa(ripoti)
itakayowasilishwa kwake Jumatano(wiki inayoanza kesho) ili imwezeshe
kutoa maamuzi yatakaondoa kuondoa mgogoro uliosababisha ujenzi Mradi wa
Bwawa la Umwagiliaji la Uluwa ushindwe kuendelea kwa sababu ya maji yake
kuelekezwa katika Msitu wa Hifadhi wa Ipembampazi.
Hatua
hiyo itasaidia kuokoa zaidi ya shilingi milioni 313 ambazo hadi hivi
sasa zimeshatumika katika ujenzi wa mradi huo ambao ni kwa ajili ya
kilimo cha umwagiliaji wa mpunga katika vijiji viwili vya Mtakuja na
Kiloleni kama mradi utaendelea.
Profesa
Maghembe alichukua uamuzi huyo jana wilayani Sikonge baada ya
kutembelea Mradi huo huku akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw.
Aggrey Mwanri ili kujionea hatua ulipokuwa umefikia na hiyo mifereji
ilijengwa kuelekea katika Msitu wa Hifadhi.
Alistaja wataalam
hao kuwa ni Ofisa wa Maliasili, Misitu, Kilimo na Mhandisi wa Maji,
Mhandishi wa Ujenzi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mteandaji wa Halmashauri
ya Sikonge ambao aliwapa jukumu la kuandaa taarifa itakayoonyesha mambo
mbalimbali ikiwemo kupima na kuonyesha kiasi cha eneo ambalo wananchi
wanalohitaji kwa ajili ya kilimo hicho na eneo lilobaki katika Msitu huo
wa Hifadhi.
Profesa Maghembe aliwaambia kuwa uharaka na ubora wa ripoti
ya Halmashauri ndio utakaoisaidi Wizara ya Maliasili na Utalii kufikia
maamuzi haraka ambayo baada ya wataalam wake kuipitia atawalisha
mapendekezo na hatua waliofikia kwa Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya hatua zaidi.
Aliongeza
kuwa wakati hatua za kupata eneo hilo zikiendelea ni vema uongozi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ukaanza kujipanga kwa kuandika andiko
la mradi wa kuomba fedha kutoka Wizara ya Maji ili kazi ya ujenzi huo
ikamilike na ianze kuwanufaisha wananchi.
Aidha
, Waziri huyo wa Maliasili na Utalii alitoa wito kwa wananchi wote
watakaopata maeneo karibu na Hifadhi mbalimbali kuwa walinzi wa kwanza
wa rasilimali hizo na kuwakemea wale wote watakaonekana kutaka
kuzihujumu kwa faida binafsi.
Kwa
upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri alisema kuwa sehemu
kubwa ya ardhi ya Halmashauri ya Sikonge ni mistu ya hifadhi ambayo
inafikia asilimia 95 na asilimia tano tu ndio inatumika kwa matumizi
mengine ya binadamu ikiwemo kilimo.
Kufuatia
hali hiyo aliwaasa viongozi wa Halmashauri hiyo kuwa makini wakati
wanaendesha zoezi hilo la kuomba eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 500 kwa
kuangalia mahitaji yao halisi ili isije ikatokea wameshapewa wanaanza tena kuomba nyongeza.
Aidha
, Mkuu huyo wa Mkoa alimweleza Waziri Maghembe, Ofisi yake
itatuma Wataalam wiwili waungane na wa Halmashauri kwa ajili ya kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa haraka na umakini ili wananchi waanze kufanikisha mradi huo.
Akisoma taarifa ya mradi huo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Abel Busalama alisema
kuwa mradi huo uliogharimu hadi sasa milioni 313 .8 ambao
ungevinufaisha vijiji vya Mtakuja na Kiloleni ulishindwa kuendelea
baada mjenzi kujenga mifereji
ya umwagiliaji akielekeza katika Msitu wa Hifadhi wa Ipembampazi jambo
lililopelekea wananchi wa vijiji hivyo kuvamia msitu na kuanzisha
mashamba ya mpunga na wengine kuingiza mifugo kwa ajili ya malisho.
Hivyo alimwomba Waziri huyo mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii kutoa ruhusa
ya eneo la hekta 500 katika Msitu wa Hifadhi ya Ipembampazi liweze
kupima na kutumika kwa shughuli za kilimo cha umwagiliaji .
Ujenzi wa mradi huo ulifika hatua ya pili ambapo ilibaki hatua ya tatu ili uanze kutumika na ndipo ulisimamishwa.
No comments:
Post a Comment