KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 16, 2017

TRUMP ADAIWA KUFICHULIA URUSI SIRI KUHUSU ISLAMIC STATE

Mr Trump (kati) akifurahia jambo na Lavrov (kushoto) na Sergei Kislyak
Mr Trump (kati) akifurahia jambo na Lavrov (kushoto) na Sergei Kislyak  
Rais wa Marekani Donald Trump alifichua taarifa zinazofaa kuwa siri kuu kuhusu kundi linalojiita Islamic State (IS) kwa waziri wa mambo ya nje wa urusi, vyombo vya habari nchini Marekani vinasema.
Taarifa hizo, zilihusu kutumiwa kwa laptopu kwenye ndege, na zilitoka kwa mshirika wa Marekani ambaye hakuwa ametoa idhini kwa habari hizo kukabidhiwa Urusi, gazeti la Washington Post linasema.
Bw Trump alikutana na Sergei Lavrov katika afisi yake wiki iliyopita.
Mshauri mkuu wa usalama wa taifa wa Marekani HR McMaster amepuuzilia mbali madai hayo kwenye vyombo vya habari na kusema ni ya "uongo".
Tuhuma kwamba huenda maafisa wa kampeni wa Bw Trump waliwasiliana na maafisa wa Urusi zimegubika utawala wa rais huyo, na kufikia sasa uchunguzi unaendelea.
Lakini rais amepuuzilia mbali tuhuma hizo na kusema ni "habari za uongo".
Wakati wa kampeni, Bw Trump alimkosoa sana mpinzani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton, kwa jinsi alivyoshughulikia taarifa ambazo zinafaa kuwa siri kuu.

Nini hasa kilitokea?

Katika mazungumzo yake na Bw Lavrov pamoja na balozi wa Urusi nchini Marekani katika afisi yake White House, trump alifichua maelezo ambayo huenda yakapelekea kutambuliwa kwa mdokezi aliyetoa habari hizo, maafisa waliambia Washington Post na New York Times.
Walizungumzia njama ya IS. Rais huyo inadaiwa alianza kuzungumzia mambo ambayo alikuwa hajapangiwa kuyazungumza, na kufichua maelezo zaidi kuhusu njama hiyo.
Njama hiyo inadaiwa kujumuisha kutumiwa kwa laptop kwenye ndege. Mazungumzo ya trump yaligusia ni jiji gani kulikuwa kumegunduliwa tishio.
Habari hizo za kijasusi zilitoka kwa mshirika wa Marekani na zilichukuliwa kuwa za usiri mkubwa kiasi kwamba hazikufaa kufahamishwa washirika wengine wa Marekani, magazeti hayo yameripoti.
Wengine waliokuwepo katika mkutano huo waligundua kosa hilo la Bw Trump na wakachukua hatua kujaribu kuzima moto huo kwa kuwafahamisha maafisa wa CIA na maafisa wa Shirika la Usalama wa taifa (NSA), gazeti la Washington Post linasema.-BBC
Donald Trump tweet from 2016

No comments:

Post a Comment