Na Mwandishi Wetu
Wadhamini
wakuu wa Ligi ya Mpira wa miguu Tanzania Bara kampuni ya Mawasiliano ya
Vodacom Tanzania PLC, jana ilitoa zawadi zenye thamani ya shilingi
232,974,660
kwa washindi mbali mbali wa ligi.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji zawadi iliyofanyika jijini Dar es Salaama jana,
Mkurugenzi Mkuu wa biashara na Masoko wa kampuni hiyo,Hisham Hendi alisema Vodacom imeongeza kiasi
cha fedha zaidi mwaka huu.
Mwaka jana tulitoa shilingi
219,502,500. Kwa ajili ya zawadi lakini mwaka huu fedha hizi zimeongezeka na kufikia shilingi
232,974,660,” alisema
Hendi
alisema, Vodacom Tanzania inavutiwa na jinsi ambavyo umaarufu wa ligi
unavyokuwa ukiongezeka siku hadi siku huku ukiwavutia na kuwaburudisha
Watanzania
walio wengi wanaoishi mijini na vijijini bila kujali kama timu za
maeneo wanayoishi zinashiriki ligi hii.
“Pamoja
na umaarufu wa ligi hii kuongezeka na mafanikio yanayozidi kupatikana,
sisi kama wadhamini tunajua kuwa bado kuna changamoto mbalimbali za
kuboresha
ligi yetu iwe na viwango vya hali ya juu na ili kuondokana na
changamoto hizi unahitajika ushirikiano mkubwa baina ya wadau wote wa
mchezo wa soka nchini japo mabadiliko hayawezi kuja kwa siku moja,”
alieleza.
Mkurugenzi
huyo alitoa wito kwa wadau wote kushiriki kubuni mikakati ya kuboresha
ligi hii na ikiwezekana wajitokeze wafadhili wengine zaidi ili
wachezaji wazidi kunufaika.
“Kama
sote tunavyoelewa hivi sasa michezo sio burudani tu kama ilivyokuwa
miaka ya zamani bali inasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuinua
uchumi wa nchi kwani wanamichezo
wakiwezeshwa wanaweza kupitia mapato yao kuboresha pato la taifa kama
tunavyosikia katika nchi za wenzetu ambako wachezaji na wasanii ni kundi
la mamilionea wanaotambulika na hapa tukiamua yote haya yanawezekana
na dalili zimeanza kuonekana.
Alisema
Vodacom itaendelea kuunga mkono na kufadhili mchezo wa soka na michezo
mingine kwa kuwa inaamini wanamichezo ni mabalozi wazuri katika
kutangaza Taifa na pia
michezo huchangia kuibua na kukuza vipaji vya wanamichezo.
“Kwa
niaba ya Vodacom Tanzania naipongeza timu bingwa ya ligi ya Soka ya
Vodacom msimu uliomalizika Yanga African bila kusahau timu zote
zilizofanya vizuri na wote waliokabidhiwa
zawadi zao leo.
Ni
matumaini yetu maandalizi ya msimu ujao wa ligi yamekwishaanza
kuandaliwa vizuri na wadau wote tutashirikiana tena kuhakikisha ubora
wa ligi unazidi kuwa bora zaidi,”
alisema Hisham.
No comments:
Post a Comment