Na Tiganya Vincent
Kahama
May 29, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amepiga marufuku minada ya ng’ombe zinazokamatwa katika Mistu ya Hifadhi kufanyika katika maeneo hayo badala yake ifanyike katika maeneo ya wazi ili kutoa nafasi kwa wananchi kushiriki kwa uwazi.
Waziri
Magembe alisema hayo juzi mjini Kahama katika ziara yake wilayani
kahama kufuatia oparesheni za kuondoka mifugo kwenye Mistu ya Hifadhi
ambapo mifugo hiyo imekuwa ikipigwa mnada ndani ya hifadhi badala ya
maeneo ya wazi.
Kwa
mujibu wa waziri Magembe utaratibu huo wa kuendesha minada ndani ya
Mistu ya Hifadhi umekuwa ukiwanyima nafasi wananchi pamoja na wamiliki
wa mifugo hiyo kushiriki katika zoezi hilo.
Alisema
kuwa wakati utaratibu huo umewafanya baadhi Maafisa waliohusika na
ukamataji wa mifugo katika eneo hilo wajihusishe na ununuzi wa ng’ombe
hizo na hivyo kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi na kushindwa kutenda haki
kwa watu wote hata wale ambao mifugo yao imekamatwa.
Profesa
Maghembe alisema kuwa kabla ya mnada haujafanyika ni vema Mkuu wa
Wilaya husika afahamishwe ili yeye na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama
iwepo wakati wa uendeshaji wa zoezi hilo ili kuondoa manung’uniko kutoka
kwa wenye mifugo na wananchi.
Waziri
huyo aliongeza kuwa ni vema kabla ya siku ya mnada kufanyika ,
Mkurugenzi Mtendaji akataarifiwa ili awatangazie wananchi wote katika
eneo lake kwa ajili ya kushiriki mnada hatua itakayoondoa malalamiko.
Naye
Meneja wa Pori la Akiba la Moyowosi Kigosi Patrick Kutondolana alisema
kuwa hifadhi hiyo inakabiliwa na tatizo kuwepo kwa kundi kubwa la
ng’ombe kutoka nchi za jirani ambazo zimekuwa zikichungwa katika eneo
hilo na ndipo ndani yake majangili utumia mwanya huo kuwinda wanyamapori
kinyume cha sheria.
Alisema
kuwa tatizo jingine ni kwa wale watu wanaopewa vibali vya kulina asali
badala yake wamekuwa wakitumia vibali hivyo kuendesha shughuli za
ujangili na kuwinda wanyama mbalimbali huku silaha zao wakiwa wakificha katika mizinga ya asali.
Meneja
huyo aliongeza kuwa wakimbizi kutoka Kambi ya Nduta mkoani Kigoma
wamekuwa wakiingia katika Hifadhi hiyo na kuendesha shughuli za ujangili
kwa kutumia silaha za kivita ambazo wametoka nazo makao kisha kurudi
makambini.
Waziri
Maghembe alikuwa na ziara katika mikoa ya Tabora, Shinyanga, Geita na
Kagera kwa ajili ya kuangalia zoezi la uondoaji wa watu waliovamia
katika maeneo mbalimbali ya Hifadhi.
No comments:
Post a Comment