Kazi hiyo inafanyika kwa ushirikiano kati ya Chuo cha Utumishi wa
Umma Tanzania na Chuo Kikuu cha Taifa cha Puntland kilichopo Jimbo la Puntland
nchini Somalia.
Mkuu
wa Chuo Dkt Henry Mambo alisema kwamba watumishi hao waliondoka nchini tarehe 3
mwezi Machi mwaka huu na wanatarajia kurejea chini tarehe 11 mwezi huu.
Dkt
Mambo alisema mafunzo hayo yanafanyika ikiwani ushirikiano kati ya Chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzania na Chuo kikuu cha Taifa cha Puntland kilichopo Jimbo
la Puntland nchini Somalia.
Alifafanua kuwa ushirikiano huo ni
matokeo ya hati ya makubaliano iliyosainiwa mwezi Mei, 2017 Makao Makuu ya Chuo
cha Utumishi wa Umma Jijini Dar es Salaam na wakuu wa vyuo hivyo viwili, Dr. Henry Mambo ambaye ni Mkuu wa TPSC na Bw. Mohamud
Hamid Mohamed ambaye ni Mkuu wa Chuo
kikuu cha Taifa cha Puntland.
Makubaliano hayo yalishuhudiwa na aliyekuwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki na Waziri wa Kazi, Vijana na Michezo wa
Puntland Mh. Abdirahman Ahmed Abdulle.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo Chuo
cha Utumishi wa Umma Tanzania
kitashirikiana na Chuo Kikuu cha Puntland kuandaa na kuendesha mafunzo
mbalimbali ya muda mfupi na mrefu ili kuwajengea uwezo watumishi wa umma wa Puntland.
Maeneo yaliyopewa kipaumbele katika uandaaji wa
mafunzo ni pamoja na;Rasilimali watu (Human
Resources Management), Utawala wa Fedha (Financial Management), Masuala ya
Manunuzi (Procurement Management),
Mengine ni Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), Mipango,
Tathmini na Ufuatiliaji, (Planning, Monitoring and Evaluation), Sera,Tafiti
pamoja na Utunzaji wa Kumbukumbu.
Mpango
huo wa Puntland unafadhiliwa na Benki ya Dunia ambao unatarajiwa kufadhili
zoezi zima la uandaaji wa mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment