Ujumbe
wa Rais mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete katikati ya wiki hii uliteka
mtandao wa kijamii wa Twitter na kusambaa kwenye Whatsapp, akionesha
sehemu ya maisha yake baada ya urais.
Dkt. Kikwete ambaye alihamia Msoga mkoani Pwani kwa ajili ya mapumziko baada ya kutoka Ikulu, aliwepa picha kadhaa akiwa anakula chakula kwenye sahani na bakuli moja na wazee ambao walihudhuria msiba wa baba yake mdogo, Said Lumaliza katika kijiji cha Msigi.
“Tukila
chakula na ndugu zangu msibani kwa baba yangu mdogo marehemu Said
Lumaliza(1917-2018) katika kijiji cha Msigi karibu na Msoga. Hii ndiyo
fahari ya maisha ya kustaafu.!” alitweet mara mbili kwa Kiswahili na
Kiingereza, Machi 8.
Watumiaji
wa mtandao huo ambao wengine walitoka nje ya nchi walisifu maisha ya
kujishusha ya rais huyo mstaafu na kueleza kuwa ni viongozi wachache
waliokuwa na cheo kama chake ambao wanaweza kurejea kwenye maisha ya
aina hiyo.
“Kuna
Maisha baada ya kustaafu. Itafika muda ulinzi kamili itakua ni yale
uliyo wafanyia watu na ndicho nilicho jifunza hapo,” aliandika Samuel
Isaya.
“Wewe
ni rais wa mfano kwa Afrika pamoja na kuwa na mapungufu yako kama
binadamu. Hongera sana mhe Mungu akutangulie ktk muda wote wa Maisha
yako,” Zakayo Sarwatt.
No comments:
Post a Comment