Mfanyabiashara,
Hariri Mohammed Hariri (45), mkazi wa Kinondoni, jana alipandishwa
katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu Tuhuma za
kusafirisha zaidi ya gramu 214 za dawa za kulevya.
Akisoma
hati ya mashtaka Wakili wa serikali, Clara Chalwe mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu Huruma Shaidi imedaiwa Machi 2 mwaka huu huko Kinondoni Matitu
ndani ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa alisafirisha
dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride zenye uzito wa gramu
214.11.
Hata
hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chohote mahakamani hapo kwa
kuwa Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za
kulevya isipokuwa kwa kibali kutoka kwa DPP.
No comments:
Post a Comment