Rais wa Urusi Vladimir Putin
ameibuka mshindi kuliongoza taifa hilo kwa muhula mwingine ujao wa miaka
sita baada ya kujipatia ushindi mkubwa.Ushindi huo ulitarajiwa katika
upigaji kura uliomalizika siku ya jumapili.Hata kabla ya kura zote
kuhesabiwa tayatri alikuwa amejizolea asilimia 76 kwa mjibu wa tume ya
uchaguzi.
Akizungumza katika mkutano wa kutangazwa mshindi amsema
ushindi wake ni matokeo ya hatua kubwa ya mafanikio aliyoyafikia katika
uongozi wake.Putin ameongeza kuwa hii ni uthibitisho wa kukubalika kwa sera zake na kwamba hana mpango wowote wa kufanya marekebisho ya katiba na kusisitiza umoja na mshikamano. "Hadi hapa sina mpango wowote wa kufanya marekebisho yoyote ya katiba,kuhusiana na unyekiti na serikali kwa ujumla.Nilikwisha sema awali kwamba nafikiria suala hilo.Lakini kuanzia leo naanza kufikiria kwa undani,kwa sababu nilipaswa kusubiria matokeo ya uchaguzi kwanza.Mabadiliko yote yatatangazwa yakifuatiwa na uzinduzi.."
"Kwangu kile mnachotaka kuniuliza inakuwa kama mizaha Fulani hivi,hebu tuhesabu,ina maana nitasalia madarakani hadi nikiwa na miaka 100? Hapana hapana hapana. " Ushindi huu mkubwa ambao ulitarajiwa,umekuwa na ongezeko la kura ikilinganishwa na ushindi wa asilimia 64 mwaka 2012.Ambapo m,pinzani wa karibu wa Putin milionea Pavel Grudinin,yeye alipata asimilia 12. |
March 19, 2018
RAIS PUTIN WA URUSI ASHINDA URAIS KWA KISHINDO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment