Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
jana amekutana na kuzungumza na Balozi mpya wa Ufaransa nchini Mhe.
Frederic Clavier ambaye aliongozana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bw. Emmanuel Baudran.
Katika mazungumzo hayo ambayo yalifanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi
Clavier aliwasilisha salaam za Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na
kusema, “Rais wa Ufaransa ana uhakika na Tanzania ijayo na anaunga
mkono jitihada za maendeleo zinazofanywa na Rais Magufuli.”
Balozi
huyo mpya wa Ufaransa nchini ambaye amekutana na kuzungumza na
Mheshimiwa Makamu wa Rais aliipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele
katika masuala mbali mbali ya Kimataifa na kusema “Tanzania ni nchi
yenye utulivu na Amani kitu ambacho kinaipa taswira nzuri Umoja wa
Mataifa”.
Mhe.
Balozi alimjulisha Makamu wa Rais kwamba Ufaransa imekusudia kuimarisha
uhusiano zaidi na Tanzania wa Uchumi na Siasa na kuanzisha majadiliano
mbali mbali katika masuala ya Mazingira,Mabadiliko ya Tabia Nchi.
Balozi
Clavier alimjulisha Makamu wa Rais kuwa mwezi ujao kutakuwa na ugeni wa
wafanya biashara kati ya 30 au 40 kutoka nchi ya Ufaransa ambao
watakuja kujionea fursa mbali mbali za kibiashara na uwekezaji
zinazopatikana nchini Tanzania.
Mhe.
Balozi alimuelezea Makamu wa Rais azma ya Ufaransa kushirikiana na Vyuo
Vikuu vya Tanzania katika kuanzisha na kuendesha kozi mbali mbali kwa
manufaa ya pande zote mbili.
Mwisho aliipongeza Serikali kwa mapambano dhidi ya rushwa na urasimu jambo litakalo wavutia wawekezaji wengi nchini.
Aidha,
Bw. Emmanuel Baudran Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la
Ufaransa alisema Shirika lao linakusudia kuanzisha kiwanda cha vifaa vya
umeme wa jua (solar) mkoani Shinyanga pia shirika hilo limeshafanya
miradi ya uboreshaji maji taka katika manispaa ya Temeke na wanaendelea
na mikakati ya uanzishwaji wa miradi mingine.
Kwa
upande wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan alimshukuru na kumpongeza Balozi wa Ufaransa kwa
kazi nzuri wanazofanya hapa nchini.
Alimhakikishia kwamba Serikali ya Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano kwa mambo yote muhimu yenye maslahi kwa wananchi.
Wakati huohuo Makamu wa Rais alikutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Mhe. Michael Danford.
No comments:
Post a Comment