Mbunge
wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya amefikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuripoti kituo kikuu cha polisi cha Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam.
Bulaya
amepelekwa Kisutu leo Jumatatu Aprili 16, 2018 ambako ameungana na
viongozi wengine wa chama hicho wanaosubiri kesi dhidi yao kutajwa.
Hivi
karibuni mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche alifikishwa mahakamani
hapo na kusomewa mashtaka matatu na kuachiwa kwa dhamana.
Heche
aliunganishwa na viongozi wengine wa chama hicho wanaokabiliwa na
mashtaka ya kuchochea chuki wanayodaiwa kuyatenda Februari 16, 2018
katika maeneo ya viwanja vya Buibui na Barabara ya Kawawa wilayani
Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Viongozi
wengine wa Chadema ambao wamesharipoti mahakamani ni naibu katibu mkuu
(Bara), John Mnyika; mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee; mwenyekiti
Kanda ya Serengeti, John Heche; mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter
Msigwa; katibu mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji; na mweka hazina wa
Bawacha, Esther Matiko.
Washtakiwa
wengine katika kesi hiyo ambao wamefika mahakamani ni mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe na naibu katibu mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu.
Kwa mara ya kwanza washtakiwa walifikishwa mahakamani Machi 27, 2018.
No comments:
Post a Comment