Baada
ya picha yake inayomuonyesha kazimia huku kashikilia kitambaa mkononi
kuibua gumzo jana mitandaoni, msanii wa filamu, Rammy Galis ameeleza
kuwa hakuwa amezimia ila alijisikia kuishiwa na nguvu.
Galis
alikuwa mmojawapo wa watu waliobeba jeneza la marehemu Agnes Gerald
'Masogange’ katika shughuli za kuuga mwili zilizofanyika viwanja vya
Leaders jijini Dar es Salaam jana Jumapili, Aprili 22.
Galis
amesema kutokana na kusimama muda mrefu wakati wa shughuli za kuuaga
mwili alijikuta akiishiwa nguvu na kuomba msaada kwa wenzie wamuondoe
eneo ilipokuwa inafanyikia shughuli hiyo.
"Unajua
nilisimama sana tangu tunapofikisha mwili pale viwanjani mpaka watu
wanaanza kuaga, nadhani kutokana na hilo nikajikuta naishiwa nguvu,
hivyo niliwafahamisha wenzangu kwamba sijisikii vizuri na kuomba
waniondoe eneo lile,”
“Hivyo
pamoja na wao kuamua kunibeba sio kwamba nilikuwa eti nimepoteza fahamu
na ndiyo maana hata kitambaa bado niliweza kukishikilia naomba watu
waelewe hivyo na kuacha kunisema kuwa nilikuwa naigiza siwezi kufanya
hivyo katika msiba," amesema msanii huyo aliyewahi kutamba kwenye filamu
ya Chausiku.
Mbali
ya kucheza filamu ya Hukumu na Masogange enzi ya uhai wake,Galis pia
alishawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu uliodumu kwa
mwaka mmoja (2016-2017).
Masogange
aliyefariki Machi 20 mwaka huu akiwa anapatiwa matibabu hospitali ya
mama Ngoma, anatarajiwa kuzikwa leo Jumatatu, Aprili 23 jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment