Katibu
wa Itikadi na Uenezi CCM , Ndg Humphrey Polepole amefunguka na kuwataka
viongozi wa vya vyama vya siasa hasa upinzani wajifunze tabia ya
kutokutoa kauli za kihalifu kwa madai wakifanya hivyo watakuwa wametenda
kosa kwa mujibu wa sheria za nchi
Polepole
ametoa kauli hiyo asubuhi ya leo (Aprili 09, 2018) kupitia ukurasa wake
maalum wa twitter wakati akijibu swali la mmoja wa wananchi ambaye
alimtaka Polepole aishauri serikali kuzipuuzia baadhi ya kauli
zitolewazo na wapinzani kwa kuziona ni za kisiasa ili kuepusha baadhi ya
mambo yanayotokea kwa viongozi wa kisiasa.
"Kauli
za kihalifu hazipaswi kupuuzwa, anayetoa kauli za kihalifu anatenda
kosa kwa mujibu wa sheria. Kauli za kihalifu ndio hufitinisha watu,
huvuruga utangamano, huleta chuki, huzaa ugomvi na migogoro. Viongozi wa
upinzani wajifunze kutokutoa kauli za kihalifu", amesema Polepole.
Aidha,
Polepole hakuishia hapo ameendelea kwa kusema "kwa sheria zetu kutusi
watu ni kosa, umtukane mtu yeyote ni kosa na nadhani ningekuwa mimi
kumtukana mtu ambaye ndiye taswira ya umoja wetu ilipasa kupewa uzito wa
ziada kiadhabu. Mazoea ya matusi yanatubomolea maadili yetu kama taifa.
Utatukaniwa mama yako halafu unachekacheka".
Tazama hapa chini uone jinsi walivyokuwa wanajibizana kati ya Polepole na mmoja wa wananchi wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment