Viongozi
wa Kitaifa kutoka Zanzibar na Tanzania Bara wamesema Watanzania
wanaendelea kumkumbuka Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kutokana na
Maendeleo makubwa aliyoyafanya wakati wa Uongozi wake miaka minane na
kufanikiwa kuacha historia isiyofutika kwa kufanikisha Mapinduzi ya
Zanzibar na tukio la kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania April
26, mwaka 1964.
Viongozi
hao wametoa kauli jhiyo jana kwa nyakati tofauti, muda mfupi baada ya
kukamilika kwa shughuli ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa
Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume iliyofanyika katika
ofisi kuu ya Chama cha Mapinduzi iliyopo Kisiwandui visiwani hapa.
Walisema
yanayooneka hivi sasa Zanzibar yametokana na dira ya maendeleo
iliyoachwa na Marehemu Abeid Amani Karume ya kuwaletea wananchi
Maendeleo katika sekta mbalimbali kwa kuondosha matabaka na kufanikiwa
kujenga umoja wa kitaifa pamoja na kuasisi Muungano ambao umevunja
rekodi kwa kudumu zaidi ya miaka 50.
No comments:
Post a Comment