Waziri
wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameweka
wazi kwamba alikuwa tayari kuchukua mashindano ya Miss Tanzania kutoka
kwa muandaaji Hashim Lundenga kwa madai kuwa kulikuwa na uhuni ulioanza
kuigubika tasnia hiyo.
Akizungumza
kwenye hafla ya uzinduzi wa Miss Tanzania Mpya chini ya Mkurugenzi wa
The Look Company, Miss Tanzania 1998 Bi. Basila Mwanukuzi, Dk Mwakyembe
amesema kuwa uhuni wa waandaji ulishamkwaza hivyo kwa kuwa mabadiliko
yameangukia mikononi mwa Basila basi anaamini 'upele umepata mkunaji'.
Akizungumzia
chanzo cha kutaka kuyaweka mashindano hayo kuwa chini yake kutoka
kwenye kampuni ya Lino Agency, Waziri Mwakyembe amesema kwamba
alikasirishwa na uhuni aliofanyiwa Miss Tanzania 2016 kwa kupewa zawadi
ya gari hewa huku akiongeza kuwa mabinti wanajitoa kwa juhudi licha ya
kuwepo kwa mfumo dume kwenye jamii.
"Watotot
wa watu wanajitolea, mfumo wetu bado ni dume wanapata tabu sana
kuishawishi jamii kuwa haya ni mashindano ya kawaida anapita kwenye
chujio anashinda alafu unampa zawadi hewa. Basila mwenyewe aliwahi
kupewa zawadi hewa kaeni naye vizuri atawaeleza. hivyo niseme mabadiliko
haya yamenifanya nione kwamba upele umepata mkunaji" Mwakyembe.
Hata
hivyo Waziri huyo mwenye dhamana ya sanaa amemtaka muandaaji huyo mpya
(Basila Mwanukuzi) kuhakikisha anaondoa ubabaishaji wote uliokuwepo na
kumuahidi kuwa serikali ipo nyuma yake.
No comments:
Post a Comment