Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya CZI Limited, Cyprian Musiba amelitaka Jukwaa la
Wahariri kujitathmini na kujitafakari kuhusiana na matamko mbalimbali
wanayoyatoa.
Ameyasema
hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodom, ambapo
amesema kuwa ni vyema Jukwaa hilo la Wahariri likajikita katika
kuwasaidia waandishi wa habari.
Amesema
kuwa Jukwaa hilo lina wajibu mkubwa wa kuwasaidia waandishi wa habari
kuboresha maslahi yao lakini si kutumika kisiasa na kuichafua serikali.
Aidha,
Musiba ameongeza kuwa TEF imekuwa ikitoa matamko mbalimbali ambayo
hayana uhusiano wowote na waandishi wa habari, hivyo ameliasa kujikita
zaidi katika kuangalia namna na kutetea maslahi ya waandishi kuliko
kutumika kisiasa.
“Press
Club hawajui, UTPC hawajui halafu wewe unatoa tamko, uandishi wa habari
sio Dar es salaam peke yake, ni Tanzania nzima, ninachowashauri TEF
tuwatengenezee waandishi wa habari mazingira mazuri ya kazi,”amesema
Musiba
Hata
hivyo, Musiba ameongeza kuwa Jukwaa la Wahariri (TEF) hawatakiwi
kulalamika kuhusu kukosa wadhamini bali wanatakiwa kujikita katika
kujenga misingi imara ya waandishi wa habari na si kutumika kisiasa kama
wanavyofanya kwasasa.
No comments:
Post a Comment