RAIS
Dk. John Magufuli anatarajia kuzindua rasmi Taasisi ya Jakaya Mrisho
Kikwete inayofahamika kwa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika
Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete ulioko Ikulu, Dar Es Salaam.
Rais
mstaafu Kikwete ndiye Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya JMKF na uzinduzi
huo rasmi utahusisha maofisa waandamizi wa Serikali, mabalozi
wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania na hasa mabalozi wa Afrika ambako
Taasisi hiyo inalenga kufanya kazi mbali ya Tanzania, wakuu wa taasisi
mbali mbali za kimataifa, wadau wa Taasisi ya JMKF, wakuu wa asasi
zisizokuwa za kiserikali (NGO’s) na wakuu wa taasisi za kijamii wakiwemo
viongozi wa dini.
Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Pioneer
Communications Limited kwa niaba ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation
(JMKF)imesema uzinduzi huo utafuatiwa na chakula cha jioni ambacho Rais
Magufuli atawaandalia wageni watakaohudhuria sherehe hiyo ya uzinduzi,
akiwemo Rais Kikwete mwenyewe na mkewa Mama Salma Kikwete.
"Taasisi
ya JMKF iliyosajiliwa rasmi mwanzoni mwa mwaka Februari, 2017, ilianza
kazi Machi, mwaka jana wakati wa kikao cha kwanza cha Bodi ya Wadhamini
ya Kimataifa ya Taasisi hiyo ilipofanya kikao chake kwenye Hoteli ya
Kilimanjaro Hyatt mjini Dar Es Salaam,"imesema taarifa hiyo.
Imeongeza
taasisi hiyo inayolenga kufanya kazi na kuelekeza nguvu zake katika
maeneo matano, itaanzia na maeneo matatu ambayo ni Afya ya Mama na
Mtoto, Maendeleo ya Vijana na Uwezeshaji wa Wakulima Wadogo katika
maeneo ya vijijini na mashambani katika jitihada zao za kujinasua katika
umasikini ama kupunguza athari na madhara ya hali ya umasikini.
"Mheshimiwa
Kikwete anasaidiwa katika uendeshaji wa Taasisi hiyo na Bodi ya
Wadhamini yenye sura ya Kimataifa ambayo wajumbe wake wanatoka nchi za
Tanzania, Marekani, Afrika Kusini, Ureno na Malaysia.Wadhamini hao ni
Balozi Ombeni Sefue aliyepata kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na Balozi wa
Tanzania katika Canada na Marekani.
"Pia
Profesa Rwekaza Mukandala aliyekuwa Makamu wa Chuo Kikuu cha Dar Es
Salaam kwa miaka mingi, Profesa William Mahalu wa Chuo Kikuu cha Mt.
Agustine mjini Mwanza na Balozi Mwanaidi Sinare Majar ambaye amepata
kuwa Balozi wa Tanzania katika Uingereza na Marekani,"imefafanua.
Wengine
ni Mfanyabiashara maarufu Abubakar Saidi Bakhressa, Balozi Charles R.
Stith aliyepata kuwa Balozi wa Marekani katika Tanzania, Msomi na
Mtumishi wa Umoja wa Mataifa Bwana Carlos Lopez, Waziri mwandamizi
katika Serikali ya Malaysia, Dato Sri Idris Jala na Mtaalamu wa Masuala
ya Fedha kimataifa Genevive Sangudi, Mtanzania mwenye makazi yake
Afrika Kusini na Marekani.
Kutokana
na kikao hicho cha kwanza cha Bodi ya Udhamini Machi mwaka jana,
wataalamu mbali mbali pamoja na washauri wa kila aina, wakiongozwa na
Mtendaji Mkuu wa JMKF, Omari Issa wamekuwa katika matayarisho makubwa
ya kuandaa nyaraka mbali mbali za msingi za kuongoza dira na dhima ya
Taasisi hiyo kwa ajili ya uzinduzi rasmi na kwamba shughuli hiyo ya
Ikulu itatangazwa moja kwa moja kwenye Televisheni ya Taifa ya TBC na
vyombo vingine.
No comments:
Post a Comment