JANA
August 08, 2018 Msanii Mkongwe wa Filamu Bongo, Mzee Majuto alifariki
dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN) alipokuwa akipatiwa
matibabu.
Kutokana
na umahiri wake katika sanaa ya maigizo kifo chake kimegusa wengi. Hiki
ni kile walichoandika Diamond Platnumz, Wema Sepetu, Ali Kiba,
Zamaradi, Ridhiwan Kikwete na Idriss Sultan kufuatia msiba huo.
Diamond Platnumz : May your Humble Soul Rest in Paradise KINGπ€΄...Will always Miss and Love youππ»
Idris Sultan:
Kazi yangu ya mwisho kama photographer/graphic designer kabla ya kwenda
BBA na ndo ilikuwa mara ya kwanza kukutana na King Majuto. Mara nyingi
alikuwa haji anaagiza watu wanatuma picha ila hii alikuja.
.
Nakumbuka
mzee aliniambia “We dogo una vituko sana ila kituko chako kikubwa
kuliko vyote ni haujui unafurahisha kiasi gani, endelea kutokujua
utashangazwa”... Sidhani kama mnajua kiasi gani unajiskia ukiambiwa kitu
kama hicho na mfalme.
To
this day nasikitika kuwa sikuwahi kumuambia alichonifanya ila naweza
kumuahidi kuwa popote nitakapoenda nitahakikisha sifanyi kosa la
kutokusema makubwa aliyotufanyia kama watoto wake kwenye comedy
industry. FOREVER A KING inna lillahi. With respect I will never call
myself KING na naomba isitokee nikaitwa pia.
Wema Sepetu : Alipangalo
Allah... I wished to work with you baba angu... Ila Allah hakupanga...
Kapumzike baba angu... Mungu Mkali jamani....πππ... Ila kama kuteseka
tu umeteseka jamani.... RIP King...
Alikiba :
Ewe Mwenyezi Mungu hakika Mzee Wetu Amri Bin Athuman (King Majuto) yuko
katika dhima yako na kamba ya ujirani wako, basi mkinge na fitina ya
kaburi na dhabu ya moto nawe ndiwe mstahiki wa utekelezaji na ukweli
msamehe na umrehemu hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa
kurehemu.AMIN.
Ridhiwan Kikwete :
“Mzee Amri Athumani Baba , Rafiki na Mzee wangu Nakushukuru kwa Maisha
Uliyoyaishi. MWENYEZI MUNGU Ana sababu katika Kuonyesha Upendo wake.
Tunakushukuru kwa Kizazi Chako Pia…Alhaj Amri Majuto. Salamu za Pole
ziende kwa Katibu Tawala Wangu wa Bagamoyo Ndg. Hamza Athumani na
Nduguze wote. Tuko pamoja sana.Pumzika kwa Amani Baba Majuto”
Aunty Ezekiel: Rip Daddy…..πππ
Zamari Mketema:
“Muda umefika Baba Safiri Salama Kikubwa umeacha Alama kubwa kwenye
Dunia na tasnia kwa ujumla Heshima yako itabaki milele PUMZIKA KWA
AMANI”
Utakumbuka
May 04, 2018 aliondoka nchini na kuelekea India ambapo alitibiwa hadi
June 22, 2018 aliporejea Tanzania na kuendelea na matibabu MNH hadi
umauti ulipomfika.








No comments:
Post a Comment