Na Ahmed Mahmoud Arusha
Kampuni
za Bima nchini zimesisitizwa kuepuka kutoa huduma kimazoea badala yake
kutoa huduma ya bima kwa makundi yaliyo sahaulika yakiwemo ya wakulima
kwa kutoa mikopo ili kufikia uchumi wa kati .
Kauli
hiyo imetolewa jana Agost 27, jijini Arusha na Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango, Dk, Ashatu Kijaji wakati alipofungua mkutano wa 41 wa Umoja
wa Kikanda wa Makampuni ya Bima ya Nchi za Mashariki na Kusini mwa
Afrika (OESAI) unaoshirikisha nchi 39.
Dk,
Kijaji alisema asilimia 75 ya Watanzania ni wakulima ambao bado hawana
elimu juu ya bima ikiwemo kupata mikopo ya bei nafuu kwaajili ya kutatua
changamoto za kilimo na kufikia katika uchumi wa kati.
Alitoa
rai kwa makampuni ya bima nchini kuangalia kundi hilo la wakulima ili
nao waweze kunufaika na bidhaa wanazozalisha kwakuwa kundi hilo ni kubwa
na ni fursa kwa makampuni ya bima nchini kuongeza idadi ya watumiaji wa
bima.
Alisisitiza
kuwa watanzania wanatumia bima ni chini ya asilimia moja idadi ambayo
hairidhishi kabisa kwakuwa watanzania wapo zaidi ya milioni 45 kwa
mujibu wa Takwimu za Taifa.
Naye
Kamishna wa Bima wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini
(TIRA) Dk, Baghayo Saqware alisema mkutano huo ni wa 41 kufanyika hapa
nchini ambapo mkutano wa mwisho ulifanyika mwaka 1995 na kusisitiza kuwa
mkutano huo unatoa fursa kwa kampuni za bima zilizopo hapa nchini
kujifunza jinsi kampuni za nje the bima zinavyofanya kazi kwa ufanisi.
Pia
kampuni hizo zitapata fursa ya kujifunza uboreshaji wa huduma kwa
kutumia mfumo wa Tehama unaoleta mageuzi katika utoaji wa huduma bora
zako bima, rasilimali watu, kuongeza wigo wa kutafuta watu mbalimbali
kwaajili ya kulipia bima ya maisha.
Naye
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo,Khamis Suleiman
alisema lengo la mkutano huo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 asilimia
50 ya watanzania wawe na aina yoyote ya bima kwani kwa sasa Tanzania
ipo kwenye nafasi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki kwa kutoa huduma
za bima.



No comments:
Post a Comment