Serikali
imetangaza rasmi kuanza kutumika kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumsihi wa Umma, PSSSF, kuanzia leo Agosti 1, mwaka huu huku sekta
binafsi watasajiliwa katika mfuko wa NSSF, ambayo itatoa mafao na
pensheni kwa wastaafu .
Akizungumza
na wanahabari jijini Dodoma jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Jenista Mhagama, alisema, Serikali imekamilisha maandalizi yote muhimu
ya utekelezaji wa Sheria ya matumizi ya mfuko wa PSSSF na imeridhika
kwamba Mfuko huo unaweza kuanza kutekeleza majukumu yake.
"Napenda
kutangaza rasmi kwamba, kwa mamlaka niliyonayo chini ya kifungu cha
1(1) cha Sheria ya PSSSF nimeteua tarehe 1 Agosti, 2018 kuwa ndiyo
tarehe rasmi ya kuanza kutumika kwa Sheria ya PSSSF", alisema Mhagama.
Kabla
ya PSSSF kuzaliwa kulikuwa na mifuko mitano ya aina hiyo ambayo ni
NSSF, LAPF, GEPF, PPF na PSPF lakini serikali kwa kutumia sheria mpya
imeipunguza mifuko hiyo na kuweka utaratibu wa mifuko miwili ambayo sasa
ni NSSF unaoshughulikia watumishi wa sekta binafsi na PSSSF ambao
wanachama wake ni watumishi wa sekta za umma.
Uundwaji
wa PSSSF kama chombo kipya kwa watumishi wa umma ulitokana na kitendo
cha Rais John Magufuli kusaini sheria namba 5 ya Mifuko ya hifadhi ya
jamii mwaka 2018, iliyosainiwa mwezi Februari iliyotaka mifuko yote kuwa
na mwangalizi mmoja ili kuboresha maslahi ya wastaafu.



No comments:
Post a Comment