Rais
John Magufuli anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa 34 wa
Jumuiya ya Serikali ya Tawala za Mitaa Tanzania (Alat). Mkutano huo
utafanyika Septemba 24 hadi 28 mwaka huu na kushirikisha wajumbe 500
wakiwemo wataalam na wageni waalikwa.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (Alat) ambaye pia ni Meya wa
Manispaa ya Shinyanga, Gulam Hafeez Mukadam amesema hayo mjini Dodoma.
Kaulimbiu
ya mkutano huo ni Umuhimu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa
Huduma na Ushiriki wa wananchi kupitia fursa na vikwazo kuelekea uchumi
wa viwanda.
Amesema
mkutano huo unalenga kubainisha mamlaka za serikali za mitaa zipo
karibu zaidi na wananchi na zinatoa huduma na kubainisha umuhimu wa
wananchi katika kubuni na kusimamia miradi ya maendeleo na kuibua fursa
za uwekezaji viwanda kufikia uchumi wa kati.
Amesema
agenda zitakazojadiliwa pamoja na mambo mengine kujadili taarifa ya
mwaka ya utekelezaji wa shughuli za jumuiya, taarifa za fedha na
kupitisha bajeti ya mwaka 2018/2019.
Makamu
Mwenyekiti wa Alat na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa, Steven Mhapa
aliitaka Alat Mkoa kufanya mikutano yao mwishoni mwa mwezi huu na
taarifa za vikao hivyo kupelekwa kwa Katibu wa Alat ili zijumuishwe
kwenye taarifa ya Jumuiya.
Meya
wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe alisema mkutano huo utakuwa
na usalama akitaka wananchi kutumia fursa hiyo. Mukadam alisema michango
ya wanachama haikuwa vizuri kwa sasa uongozi wake umejipanga
kuhakikisha wanachama wake wanalipa madeni.
"
Tumepanga kuweka mazingira ya kuhakikisha wanachama wanatoa michango na
hii si kwa ajili ya mkutano huo pekee bali kuhakikisha wanajenga jengo
la kitega uchumi jijini Dodoma kwa ajili ya wana Alat," amesema na
kuongeza mkutano huo utagharimu sh milioni 300.



No comments:
Post a Comment